MSAKO wa Fisi
waliovamia makazi ya Vitongoji vitatu vya Kijiji cha Hungumalwa Kata ya
Hungumarwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, umezua maajabu.
Maajabu hayo
yamehusishwa na imani za kishirikina, baada ya fisi wawili kati ya 12
waliouawa, kukutwa wamevalishwa shanga na Rozali, kiunoni.
Msako huo
wasiku tatu ulioanza juzi (Jumapili) unahusisha mamia ya wananchi wa Kijiji
hicho na vitongoji vyake vya Mwanzabalemi, Mwanega na Mwang’ombe, wanaotumia siraha
za jadi na mbwa wapatao 50.
Habari za ndani kutoka Kijijini humo zimesema
kwamba, kabla ya wananchi hao kuingia ‘vitani’ kusaka wanyama hao ambao baadhi
wanadaiwa kumilikiwa na watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina,
wazee wa Kijiji na Vitongoji hivyo, walifanya mazindiko (kinga) ya kujikinga na
nguvu za washirikina ambazo zinge kwamisha zoezi hilo.
Kwa mujibu
wa baadhi ya wazee wa kijiji hicho ambao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema kuwa makamanda wa jadi wanaoongoza msakao huo pamoja na mbwa wao, wana
kinga za kupambana na imani za kishirikina vinginevyo wasingeweza kuua fisi
wenye shanga na Rozali wanaotumiwa kishirikina.
Diwani wa
Kata ya Hungumalwa Shija Malando akizungumza na waandishi katika Kijiji hicho
jana, alisema wananchi walifikia maamzi ya kufanya msako huo wa siku tatu, baada
ya kundi kubwa la Fisi hao wanaokadiliwa kuwa zaidi ya 80, kuwa tishio kwa
watoto na mifugo.
Alisema
kuwa, kwa muda wa miaka miwili iliyopita hadi sasa, licha ya wanyama hao
kuharibu hekali moja ya matunda aina ya Tikiti Maji yaliyokuwa yamelimwa na
mwanchi mmoja, wameua ng’ombe 109, Mbuzi 135, kondoo 127 na Nguruwe 15 katika
Vitongoji hivyo.
“Njooni
muone maajabu haya.” Alisema Malando na kufafanua “Jana (juzi Jumapili)
wananchi walifanikiwa kuua fisi kumi wawili kati yao wakiwa na maajabu. Mmoja
aliukuwa na Rozali kiunoni na mwingine akiwa na shanga kiunoni huku uume wake
ukiwa umetahiriwa kama binaadam.”
Alisema fisi
waliokutwa na vitu hivyo kiunoni, kwa imani za kabila la Kisukuma, wanadaiwa kumilikiwa
na baadhi ya watu wenye imani za kishirikina na kwamba, waliuawa majira ya saa
8 hadi saa 10 mchana kwenye eneo la mlima wa Mwanzabalemi.
Alifafanua
kuwa, fisi kumi waliuawa (jumapili) siku ya kwanza ya msako huo na wengine
wawili waliuawa jana asubuhi na kwamba maeneo ya milima ya Mwanangi katika Kijiji
cha Buyobo na Kitongoji cha Mwanzabalemi yanasadikiwa kuwa na fisi wengi zaidi.
“Pamoja na
kushambulia mifugo wetu, ilifika mahali wananchi walikuwa hawawezi kutembea kwa
uhuru nyakati za usiku na baadhi ya watoto wanaosoma mbali kukatisha masomo kwa
kuhofia kuliwa na fisi hao.” Alieleza Mwenyekiti wa Kijiji cha Hungumalwa,
Clement Kaswahili.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Mwang’ombe Joseph Kisena alisema hadi kufikia leo (siku ya
tatu ya msako huo) watakuwa wameua fisi wengi zaidi kutokana na ushirikiano
mzuri wa Vitongoji hivyo vinavyotumia mbwa 50 na siraha mbalimbali za jadi ikiwemo
mikuki, mapanga na marungu.
Kisena alisema,
pamoja na maajabu ya fisi kuvaa shanga na Rozali kiunoni ambayo wamejionea na
kuzua imani za ushirikina kwa baadhi ya wananchi, hawatarudi nyuma, hadi
walitokomeze kundi la wanyama hao ambalo ni tishio kwa wananchi na mifugo wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.