Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam. |
BIA
YA SAFARI LAGER YASHINDA TUZO LA UBORA KIMATAIFA 2014
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar
es Salaam, Alhamisi 29Mei 2014;Kampuni ya Bia Tanzania(TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza ushindi wake wa tuzo la Ubora
wa Kimataifa 2014 maarufu kama ‘International High Quality Trophy 2014’ katika
mashindano ya Monde Selection. Safari Lager itapokea tuzo hiyo Jumatatu tarehe 2
Juni, mjini Bordeaux, Ufaransa.
Tuzo ya Ubora wa Kimataifa au ‘International High Quality
Trophy’ ni tuzo ya heshima linalotolewa kwa bidhaa ambazo zinashinda tuzo za
‘Gold’ au ‘Grand Gold’ kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo. Safari Lager inepewa
tuzo hiyo ya heshima kwa kuweza kushinda ‘Gold’ na ‘Grand Gold’kwa zaidi ya
miaka mitatu mfululizo.
Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Bw. Oscar Shelukindo,
alisema, “Safari Lager ni bia ambayo siku zote nia yake ni kuridhisha
wateja wake na kwa miaka yake yote…Tunaishukuru sana Monde Selection kwa
heshima waliyotupa nahii inatupa motisha ya kuendelea kuwapa wateja wetu bia
bora zaidi”.
Bw. Fimbo Butullah, Maneja Masoko wa Safari Lager
aliongezea kwa kusema, “Tungependa tena kuishukuru Monde Selection kwa heshima
waliyotupa, wateja wetu na kwa Watanzania kwa ujumla. Sisi Kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kufika hapa tulipo sifa hizi si za TBL
peke yake ni za Watanzania kwa ujumla na haswa wateja wtu wanaotumia bia ya
Safari Lager”.
Fimbo alimaliza kwa
kutoa wito kwa wateja wa Safari Lager kuendelea kutumia bia hiyo kwani
ndio bia namba moja kwa ubora na kwa mauzo Tanzania na pia ni bia namba moja
Afrika na leo hii tunapozungumza imepata heshima ya pekee ya ubora wa
kimataifa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.