Taarifa za awali zinaeleza kuwa basi hilo liliacha barabara na kugonga nyumba ambapo lilipinduka na kusababisha vifo hivyo huku idadi kubwa ya abiria wakijeruhiwa vibaya.
Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Magu na wengine katika Hospital ya Rufaa Bugando huku kukiwa na taarifa ya idadi ya watu waliopoteza maisha kuongezeka hadi kufikia jioni hii.
Miongoni mwa abiria waliokuwemo katika basi hilo ambao wamepoteza maisha ni Pamoja na Alex Masatu (Dj Alex da Wolf) ambae alikuwa ni mfanyakazi wa Radio Metro iliyoko Mkoani Mwanza.
Taarifa zaidi tutaendelea kukuwasilishia kadri zitakavyo tufikia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.