ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 5, 2014

TSN BOYS KUKABILI MWANANCHI MEDIA KOMBE LA NSSF KESHO: MROKI AIAHIDI DAU NONO.


Kikosi cha TSN Boys

TIMU ya soka ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo vya Habari 2014.

Mechi hiyo itakayochezwa LEO (jumamosi) saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.

TSN imetinga hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa mabao 9-0.

Mwananchi ni mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.

TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu"  ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000. 

"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.

Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo. 

Katika mechi za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo JANA walitolewa baada ya kufungwa mabao 2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.

Bao la Jambo JANA lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo mazuri (best looser).

Katika netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao 19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
mabao 27-8.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.