Tanzania na Diaspora.
Wakati watanzania tunaendelea kushuhudia kikao cha
marekebishia ya Katiba kikiendelea
napenda kujumuika na baadhi ya waliopata nafasi kuchangia kuhusu swala la
uwezekano wa uraia wa nchi mbili (Due citizenship).
Katika ya nchi yetu tuipendayo kwa sasa haitambui uraia
wa nchi mbili, kwa maana kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine unapoteza haki
ya kama raia wa Tanzania, Swala hili linapaswa kuangaliwa kwa makini wakati huu wa
marekebisho ya katiba, Kwa maoni yangu iwe ruksa kwa Mtanzania kuwa na uraia wa
Tanzania hata kama utakuwa umechukua uraia wan chi nyingine, swala hili
lisipoangaliwa makani ama likiangaliwa haraka haraka linaweza tafsiriwa kuwa watanzania
hao wanatamaa ya kutaka huku na kule, si sahii kulitafsiri namna lightly namna hiyo,
wengi wa watanzania waliokwenda kuishi kasha kuombauraia kuishi nchi nyingine
hawakuwa na maana wa kuukana Utanzania na ukiangalia mpaka sasa hakuna anayetamba
ama kuupondda U-Tanzania popote alipo.
Wengi wa watanzania wanaoishi ughaibuni ama nchi yoyote
nje ya Tanzania na kupata uraia wa nchi hiyo bado wanajitambulisha kama
watanzania, uraia wanaopewa ni haki ambayo wengi wao wameifanyia kazi muda
mrefu sana katika nchi waliyopo, na ili kupata baadhi ya haki muhimu inabidi
watambulike kama raia, kwa maana hiyo inabidi kuomba uraia wan chi waliyopo,
lakini hii haimaanishi hata kidogo kuwa sasa Tanzania basi. Hata watanzania
waliokuwa wakubwa kisiasa waliishi nje lakini inafika wakati wanarudi nyumbani
kama kina Abrahaman Babu na Mzee Kambona nyumbani ni nyumbani huna ujanja.
Watanzania hao amabao baada ya kupata uraia wa nchi
wanayoishi sasa wanatakiwa kuomba visa kuingia
Tanzania, yani Mswahili wa Tarime au Ndanda sasa wanakuja Tanzania kama mgeni!,
wanalipishwa kiingilio kwa dola katika mipaka yote ya Tanzania. Kuwapa haki
katika nchi yao mama (Tanzania) ni swala muhimu katika kuendeleza Tanzania pia,
maana yangu ni kuwa wengi wanafanya kazi
nje ya nchi lakini mawazo yao ni Tanzania wengi ama wote wanandugu ambao bado
wanawasiliana nao kila mara, katika kuwasiliana huko wengi wanawekeza Tanzania
sababu ndio kwao na ndipo siku wakikata kauli wengi watarudishwa na kulazwa
walipolala ndugu zao wengine.
Raia wengi tunajua ugumu wa Maisha yaliyopo Tanzania tuna
wahitimu wengi ambao wanamaliza na kufaulu vizuri bila kupata ajira, wapo wenye
bahati ambao humaliza na kuanza kazi moja kwa moja lakini wengi hawana bahati
hiyo. Mtanzania ambaye amekwenda kujiendeleza nje analiona hili swala na anajua
labda hayupo kwenye kundi la wenye bahati kwa maana kuwa atarudi nyumbani na
hakuna ajira na wanaopata ajira wengi kama walimu wanaanzia mshahara wa
shilingi 277,00=, kiasi ambacho ambacho ukijiuliza mwalimu huyu ambaye amepanga
na kutumia public transport anafikaje mwisho wa mwezi hupati jibu, ukipata bahati
unaweza anzia taasisi zinazolipa 750,000= kwa mwezi, lakini ni watanzania
wangapi wanabahati hiyo?.
Nchi kama Uholanzi mshahara wa mwezi unaanzia Euro 1440
sawa Tsh 3,240,000 Norway wanaanzia euro
2000 na Uingereza ni zaidi ya hapo, kwa haraka haraka watu hawa wanaweza kuishi
kwa amani huko walipo nabado wakasaidia ndugu zao ambao wapo Tanzania.
Nchi kama uingereza ukiwa raia una haki kuishi kwa
kutegemea Serekali kwa chakula malazi ,matibabu yaani hata kama hufanyi kazi,
kwa maana hiyo Mtanzania huyu akipata kazi na anaishi nchi ambayo kwa kawaida
huwezi kujinunulia kiwanja na kujenga unless uwe Millionea siku zote atakuwa na
mawazo ya kuja kuijenga nyumba yake nyumbani na ya kisasa kama anayoiona huko
nje, na kwa vile anaishi nje basi hii nyumba yake wataishi watanzania ambao
kama walivyo wengi wetu hawana uwezo wa kujenga kwa haraka na kwa mishahara
halali. Tutakaporuhusu Mtanzania anayepata uraia nje kuendelea na uraia wake wa
Tanzania kama atapenda basi ataendelea kulala na kuwaza Tanzania.
Mimi nimeishi nje ya Tanzania kwa muda sasa kwahiyo naelewa umuhimu wa kuendelea
kuwa raia wa Tanzania, naelewa umuhimu wa siku moja kuja zikwa pale walipozikwa
ndugu zangu.
Wajumbe wa Bunge wa katiba watumie busara katika kujadili
hili swala bila kusahau kuwa watanzania wanaoishi je na wamepewa uraia huko wanapenda
kuendelea kuwa watanzania, wajumbe watakuwa wametenda jema kuruhusu uraia wa nchi
mbili hasa kwa watanzania waliobahatika kupata uraia wa nchi nyingine katika
njia ya kutafuta maisha kwa ajili yao wenyewe na ndugu zao.
Sababu nchi nyingi wanazoishi Wazanzania nje ya Tanzania
system yao ya kufanya kazi ni 100% kazi hivyo watanzania wengi wanajifunza na
kunakili mifumo hiyo ili siku wakirudi nyumbani wawaambukize watanzania wenzao
maana nchi nyingi za nje unaposema kazi unamaaninisha kazi na si kazi ya
kuingia saa unayotaka na kusign na kuondoka, unakula kwa jasho lako kihalali na
ukijituma unapata, Japo ni kidogo lakini
watanzania walio nje wanaweza na wamekuwa wakichangia kihalali kidogo walicho nacho
katika kuendeleza uchumi wa Tanzania wengi wakati wa mapumziko huja Tanzania na
wengi wao hawaji mikono mitupo ama hawaji kutengemea ndugu za walioko Tanzania
badala yake huja wamekamilika na vitu ambayo wengi huvituma bandarini na
kulipia ushuru, siku wakiwa wanaondoka kurudi makazini wengi wao huondoka
watupu na kuanza upya katika arakati za kukusanya ili akirudi tena Tanzania aendelee
pale alipoachia mara ya mwisho.
Mtanzania
anayeishi nje hana sehemu ya kuishi kwa furaha zaidi ya Tanzania, hana sehemu
anayoishi kwa amani zaidi ya Tazania, Mtanzani huyu hana sehemu aliyo na
marafiki wengi zaidi ya Tanzania,
Mtanzania huyo ambaye wazazi na ndugu zake wote wako Tanzania leo anaadhibiwa
kwa kitendo cha kwenda kutafuta kipato ambacho hakipereki popote bali Tanzania.
Miaka ya sabini ilikuwa inaeleweka pale alipoadhibiwa
mtanzania aliyekwenda kusoma Urusi, Denmak,
Hungary na akakataa kurudi, sababu tuliitaji wataalam wetu ambao
hatukuwa nao wa kutosha na wengi wao waliperekwa na gharama za serekali, Zanzibar
tulikuwa na chuo kimoja tu tena cha ualimu pekee na sasa kuna vyuo zaidi ya
vitatu vikubwa,bara kulikuwa na chuo kikuu kimoja
tukilicho kuwa kinahitimisha wanafunzi 15 tu
na sasa tunavyuo zaidi ya 30 wanaohitimu ni zaidi ya 110,000 kwa
mwaka, kwa miaka hii wengi wako
nje kwa gharama zao katika kutafuta kilicho bora kwa ajili ya watanzania wenzao
na sasa akifanikiwa kupewa uraia na nchi husika ili aishi kwa amani na haki
zote za kufanya kazi kusoma nk Tanzania inamwambia sasa hapa ni wewe ni mgeni
ukija kumuona mama ama baba yako ama kuendeleza nyumba yako unayojenga kijijini
kwenu kule Butiama basi lipa kiingilio (visa)!!.
Watanzania walioko nje hawako nje sababu hawaipendi
Tanzania na anafikiria hiyo atakuwa anajidanganya, Tanzania iko miyoni mwetu na
hata serikali ingeweza hata ingeruhusu tukatengeneza system ya kupiga kura
wakati chaguzi kuu zinapowadia. Wawakilishi wa vyama vya siasa katika bunge
hili lililopewa heshima ya kurekebisha
katiba tunawaomba kuingiza swala hili
katka katiba mpya, Mheshimiwa Membe amekuwa akisikiliza na kwa makini kilio
hiki cha watanzania walioko nje, pia mheshimiwa Kikwete amekuwa akikumbana na
hili ombi kila wakati akikutana na watanzania waishio nje, katika kikao chake
cha mwisho na watanzania Uingereza pale Wembley Mheshimiwa Raisi alisema swala hili
limeingizwa kwenye rasimu kwahiyo liko ndani ya bunge kujadiliwa, napenda
kumpongeza Mh Dr Kikwete kwa kutambua kilio hicho mpaka kumteua Singo
kuwakilisha diaspora (thank you Mr President) katika kikao hicho.
Lakini sababu kwa
walio wengi swala hili si muhimu kwao huko bungeni tunaomba mfungue macho na
kulipa umuhimu. mnapojadili mjue mnamuongelea Masatu, Juma, Asha, Owino, Yasunta
na wengi ambao huko waliko japo wamepewa uraia lakini wanahesabiwa kama wageni
hawatakubalika kama wenyeji unless wameishi zaidi ya miaka 30, mjue mnamjadili
mtu ambaye anakuja Tanzania sio kuchuma ama kujifunza Kiswahili na mila za
Tanzania la hasha mnajadili maisha ya mtu amabaye amewaachia watanzania wenzake
nafasi za ajira Dar , Mwanza ama Ndada na kwenda kutafuta huko nje ya nchi na anachopata
japo kidogo lakini anakula na wakwao –WA-TANZANIA.
Mungu bariki Tanzania yetu.
Peter H.A. Owino
Rorya
Tanzania.
Live in UK
Peter H.A. Owino
Rorya
Tanzania.
Live in UK
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.