6 MACHI, 2014
CHADEMA JIMBO LA CHALINZE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Demokrasiana Maendeleo
(CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani wa kupata mgombea ubunge
kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Aprili, mwaka
huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi Jimbo, kuanzia tarehe
4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa tarehe 7 Machi
2014, saa 10.00, jioni.
Kura za maoni ndani ya chama, zitafanyika
tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa na kikao cha kamati ya utendaji
ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu wa Katiba ya chama na hatimaye kikao
cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili kupata mgombea atakayeshindana na wagombea
wa vyama vingine.
Mpaka sasa wagombea waliochukua fomu
kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea wengine watatu (3) wamechukulia
fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, hivyo hadi sasa idadi ya wagombea
waliotambuliwa rasmi ni sita.
Tunatumia nafasi hii kuujulisha
umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa fomu za kuwania uteuzi
wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu ya Chama, Ofisi ya
Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama www.chadema.or.tz
Imetolewa Machi 5, 2014
Iddi Omary Ucheche
Katibu wa CHADEMA, Jimbo la Chalinze
0756 639014
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.