ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 6, 2014

WASHINDI WA PROMOSHENI YA MIMI NI BINGWA WAIPONGEZA AIRTEL.

Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa mmoja kati ya washindi wa milioni moja Bw. Ramadhani Wefa mkazi wa Kinondoni jijini Dar es salaam.Zaidi ya shilingi milioni 150 zimeshatolewa kwenye promosheni hiyo.
Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia) akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa mmoja kati ya washindi wa milioni moja Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi ya kwenda kushuhudia moja kati ya mechi za Manchester United nchini Uingereza kwenye uwanja wa Old trafford.Mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 150 zimeshatolewa kwenye promosheni hiyo.
Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (wa pili kushoto) akiongelea umuhimu wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi baada ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa baadhi ya washindi wa promosheni hiyo (waliopo pichani). Kushoto ni Bw. Ramdhani Wefa, Kulia ni Philemon Nathaniel Mgaya akifuatiwa na Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi na wote wakiwa wanatokea Dar es salaam.
Washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa waipongeza Airtel

WAKATI Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel ikisubiria kuchezesha droo kubwa ya shilingi Milioni 50 kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa, baadhi ya washindi waliokwishapatikana wamejitokeza wakiisifia kampuni hiyo kwa kuratibu promosheni zenye kulenga maendeleo kwa watanzania walio wengi nchini.

Washindi hao wameainisha hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa pesa zao mapema wiki hii kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel ziilizopo Morocco jijini Dar es salaam.

Washindi hao wamedai kuwa mara nyingi watu huwa hawaamini promosheni zinazoendeshwa na kampuni ya simu kama Airtel na hivyo kujikuta wakibaki nyuma kwa kuogopa kuthubutu.

“Mi binafsi sikuwahi kumuambia mke wangu kwamba nashiriki kwenye promosheni ya Mimi ni Bingwa sababu huwa akijua nashiriki ananikasirikia na kusema nina matumizi mabaya ya pesa, lakini leo nimeibuka mshindi wa shilingi milioni moja yeye akishuhudia na vilevile nimeshinda tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford,” alisema mshindi huyo Bw. Msemwa Makuzi mkazi wa Dar es salaam.

Mshindi huyo aliendelea kwa kusema, kwa hali ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuamini kwamba ameshinda shilingi milioni Moja na tiketi ya kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.

“Kweli mimi kama mtu mwingine yeyote wa kawaida iliniwia vigumu kuamini kwamba nimeibuka mshindi wa pesa hizo na tiketi. Na imenichukua muda kuamini mpaka sasa baada ya kukabidhiwa hizi milioni moja ndo naamini kweli mimi ni mshindi,” alimalizia Bw. Makuzi.

Aidha washindi wengine wamewaasa wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi katika promosheni hiyo kwani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa zima.

“Kwa kweli mi nawaambia watanzania wenzangu wasidhani hivi vitu ni masihara, watu wanashinda kweli na maisha yao yanabadilika kupitia hizi pesa tunazopewa. Mimi hapa naiwinda hiyo milioni 50 kwani nina uhakika nikishinda nitakuwa nimesahau kabisa umasikini,” alisema Ramadhani Wefa ambaye ni mshindi wa milioni moja kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema bado Airtel inatambua na itaendelea kutambua umuhimu wa wateja wake hivyo haina budi kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye manufaa kwa wananchi wote kiujumla.

“Airtel inaelewa fika kuwa wateja ndio kiini cha maendeleo ya kampuni hiyo na hivyo inajitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora za kuwanufaisha wateja wake na kuleta maendeleo kwa taifa zima kiujumla,” alisema Jane.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.