ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 12, 2014

MWENDESHA PIKIPIKI AFA KWA KUGONGWA NA LORI LA COCA COLA JIJINI MWANZA.

PICHA NA SAUTI ZAJA HIVI PUNDE.
Watu wanne wameripotiwa kufariki dunia  katika matukio manne tofauti mkoani Mwanza  vikiwemo vifo vilivyo sababishwa na ajali za barabarani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza  Valentino Mlowola amesema Katika tukio la kwanza mtu aliyejulikana kwa jina la Japhery Reluwe  mwenye  umri kati ya miaka 25-30 mkazi wa Tanesco  amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya balloon  katika barabara ya Kenyata –Maliasili.

Katika tukio jingine mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake anaesadikiwa kuwa na umri wa  kati ya (20-30)  aliuawa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto na kundi la wahalifu katika eneo la kiloleli kata ya nyamanoro wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Aidha mapema Leo Mtu mmoja ambaye pia hakufahamika jina lake amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 442 BSH mali ya  kampuni ya Nyanza Botling Company Ltd (Cocacola) ya jijini Mwanza na pikipiki aina ya Sanya yenye namba za usajili T 115 CKP  mali ya Aristides Fidelis .


Ajali hiyo ambayo imetokea katika eneo la taa za kuongozea magari barabara ya Nyerere na hatimaye gari hilo kuungua moto, imesababisha kifo cha abiria aliyekuwa  katika pikipiki ambaye hajafahamika jina lake  na  mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.