ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 26, 2014

YANGA YAKABIDHI KADI 9 TAWI LA MWANANYAMALA

Mlezi wa tawi la Yanga la Green Stone lililoko Mwananyamala , Yusuf Mwandeni akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa tawi hilo, Michael Machellah wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika Ukumbi wa  CCM Mwinjuma Dar es Salaam jana.
Mwanachama mpya wa Yanga, Michael Machellah akifurahia kadi yake ya uanachama wa Klabu ya Yanga mara baada ya kukabidhiwa na mlezi wa tawi hilo, Yusuf Mwandeni (wa tatu kushoto) wakati wa hafla fupi ya tawi hilo iliyofanyika katika Ukumi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wanachama wa Yanga,tawi la Green Stone la Mwananyamala wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam jana, katika picha hii pia anaonekana mwanamuziki mahiri wa dansi nchini Muumini Mwijuma (mwenye T.shirt ya njano wa kwanza kulia mstari wa mbele) .




Baadhi ya Wanachama wa Yanga,tawi la Green Stone la Mwananyamala wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam jana.


Yanga yakabidhi kadi 9-Tawi la Mwananyamala
Na Mihael Machellah
TAWI la Yanga la Green Stoni lenye makazi yake Mwananyamala CCM Mwinjuma jana limekabidhi kadi tisa kwa wanachama wake wapya ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mlezi wa tawi hilo la Green Stone mara baada ya kukabidhi kadi hizo, Yusuf Mwandeni alisema tawi hilo mpaka sasa lina jumla ya wanachama hai na wenye kadi 45 tangu lianzishe mwaka 20012.

Mwandeni alisema tawi hilo kwa sasa liko katika harakati ya kuhamasisha wapenzi na mashabiki wa timu ya Yanga wachukue kadi na waichangie Klabu yao kwa kupitia kadi za uanachama na njia nyinginezo.

Tawi la Green Stone linatarajia kufanya uchaguzi wiki ijayo Februari 2,2014 katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa nafasi ya Mwenyekiti,Katibu,Mwekahazina,Msemaji wa tawi na wajumbe wa kamati kuu ya Tawi.

Nae Mwenyekiti wa Tawi hilo, Lumole Matovolwa aliushukuru uongozi wa Yanga kwa timu kuipereka Uturuki na juzi imeonyesha mambo mazuri ambayo wameyapata huko baada ya kushinda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ashanti United lakini pia aliitakia timu maandalizi mema na mazuri kwa yote wanayokabiliana nayo hivi karibuni tawi la Green Stone liko nyuma yao kwa sapoti ya namna yoyote.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.