Ikiwa zimesalia siku mbili tu kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Toto Africans ya jijini Mwanza, hatimaye leo tena ikiwa ni mara ya tatu sasa, Club hiyo imetangaza kuuahirisha uchaguzi huo ikitangaza kuanzia leo kuanza rasmi zoezi la utoaji fomu za uchaguzi kwaajili ya wanachama halali watakao hitaji kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Toto Africans.
Awali TFF iliitaka Toto Africans kukamilisha uchaguzi wake kabla ya tarehe 30 ya mwezi huu (January) lasivyo itakutana na adhabu kali ya kushushwa daraja ambapo Club hiyo ilipanga uchaguzi wake kufanyika tarehe 26, lakini sasa kutokana na kukwamishwa na baadhi ya mipango iliyo hitaji fedha hasa ukizingatia kuwa wanachama wengi wamemaliza fedha zao kwa sikukuu na ada kwa watoto, Toto Africans imeamua kuusogeza mbele uchaguzi wake hadi tarehe 7/02/2014. BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.