ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 11, 2013

KAMPUNI YA VILAINISHI YA ORION YAINGIA UBIA NA KAMPUNI YA CHEVRON KUSAMBAZA BIDHAA ZAO.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Orion Lublicants, Beny Maregesi akizunumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuchaguliwa kwa kampuni hiyo kuwa wasambazaji wa Oil za Caltex nchini Tanzania.Hafla hiyo ilifanyika DAR ES Salaam jana.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizunumza na wagwni waalikwa(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuchaguliwa kwa kampuni hiyo kuwa wasambazaji wa Oil za Caltex nchini Tanzania.Hafla hiyo ilifanyika DAR ES Salaam jana.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kampuni ya vilainishi ya Orion yaingia ubia na kampuni ya vilainishi ya Chevron kusambaza bidhaa zao
Bidhaa za Caltex zimerudi sokoni baada ya kuwa nje soko tangu mwaka 2010
Dar es Salaam, Tanzania, December 5, 2013 – Kampuni ya vilainishi Orion, leo wameingia ubia wa kusambaza bidhaa za wamiliki na watengenezaji wa vilainisha injini Chevron. Kampuni za vilainishi Texaco na Caltex ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza kwenye kwenye teknolojia ya mafuta duniani. Makubaliano haya yanaifanya kampuni ya vilainishi ya Orion kuwa msambazaji pekee wa vilainisho vya Chevron kwa bidhaa yake Caltex.

Vilanishi vya Chevron kupitia Orion ina mpango wa kukuwa na kurudisha heshima yao ya kuongoza katika utoaji wa vilainisho bora. Kampuni ya Orion kwa sasa ndio kampuni pekee yenye mamlaka ya kusambaza bidhaa za Caltex pamoja na bidhaa maarufu za Delo and Havoline, vile vile Orion watatoa huduma za vilainisho viwandani na majini.

Tamko hilo lilitolewa kwenye chakula cha usiku kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ukiuzuliwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya Orion Maregesi Manyama, meneja biashara Clint, Nickall,na wadau wengine kwenye tathiniya hii.

“Soko la Tanzania limekuwa kwa kiasi kikubwa na tumegundua kuna hitaji ya vilainishi halisi na huduma bora alisema Maregesi Manyama wa Orion”.  “Vilainishi vya Caltex vimerudi tena Tanzania na muda muafaka baada ya ripoti TBS ya hivi karibuni kuonyesha kwamba asilimia tisini ya vilainisho nchini havina ubora. 

Tunatazamia kuwa na mahusiano ya mda mrefu na kampuni ya vilainishi ya Chevron, kwani watatupa misingi ya ufahamu kuhusiana na vilainisho bora na kuifanya bidhaa ya Caltex kuwa chaguo la watanzania”.

“Tunashukuru kwa ushurikiano huu na kampuni ya vilainishi ya Orion na kupanua wigo wetu kutoa vilainishi bora barani Afrika.” Aliongeza Clint Nickall wa kampuni ya vilanishi ya Chevron.

Bwana Nickall aliendelea kwa kusema “Katika uchaguzi wao wa kumpata mshirika ambae atawasambazia bidhaa zao kampuni ya Chevron walikuwa makini na kuwa na imani na kampuni ya vilainishi ya Orion itaweza kuwapatia wateja vilainishi na huduma bora”.
Kuhusu Orion
Kampuni ya Vilainishi ya Orion yenye makao yake jijini Dar es salaam, Tanzania. ofisi zao zipo Mandela Road Buguruni. Orion wamechaguliwa kuwa wasambazaji wa kampuni ya vimiminika ya Caltex ambayo itajumuisha bidhaa za Delo Havoline. 

Mtendaji mkuu wa Orion Maregesi Manyama ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kwenye nishati na ameshika nyazfa mbalimbali ndani na makampuni ya mafuta ya kimataifa. Bodi ya vilainishi ya kampuni ya Orion inaundwa na watu wanaojua vizuri vilainishi. 
Kampuni ya vilainishi ya Orion Kwa maelezo zaidi kuhusu Orion na wakurugenzi wake tembelea tovuti ya www.orion-lubricants.com

Kuhusu Chevron
Chevron ni kampuni inayoongoza katika kutoa nishati bora. Mafanikio yetu yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na watu wetu kwa kujikita katika utoaji wa bidhaa bora kwa lengo la kupata matokeo chanya, hivyo basi katikaupatikanaji wa mafanikio haya huduma zetu zimekuwa ni za viwango vya juu, vile vile utumiaji wetu wa  teknolojia bora na kutumia fursa kwa lengo la kupata faida. 

Tupo karibu na tathiniya hii ya nishati. Tunatengeneza, kuzalisha na kusafirisha mafuta na gesi, vile vile tunachuja mafuta na kusambaza vilainishi, tunatengeneza na kuuza nishati ya petrochemical na nishati mvuke tunazalisha umeme na kutoa nishati mbadala na kutengeneza nishati kwa ajili ya baadae, vilevile tunafanya utafiti nishati ya mimea ya juu.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti www.chevron.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.