ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 19, 2013

HUYU HAPA MWANDISHI WA HABARI MUONJAJI BORA WA BIA MWANZA 2013-2014.

Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Willy Mlinda, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka likiwa na nia ya kudumisha mahusiano baina ya kiwanda hicho na wanahabari.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Moses Mathew wa Mwananchi Communication, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza. 
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Charles Masamba, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza.
Awali kabla ya shindano la uonjaji bia,  Mpishi mkuu wa Kampuni ya Bia TBL tawi la Mwanza Oscar Kilasi alitoa somo kwa waandishi hao juu ya kuzibaini tofauti za bia kupitia ladha, rangi, harufu na viwango vya alcohol.
Naye Afisa Ubora wa bia za TBL tawi la Mwanza Jeremiah Kamambi alitoa somo Wajibu wa Muuzaji na Mnywaji wa bia likiwemo suala la kuzingatia afya na umri sahihi kwa watumiaji kileo.
Afisa Mahusiano wa TBL Tanzania Doris Malulu akizungumza na wanahabari dhamira ya Kampuni yake kuliendeleza shindano hilo kwa kuliboresha miaka baada ya miaka ikiwa ni pamoja na ndoto ya kulifanya shindano hilo kuwa la kitaifa zaidi kwa wadau wa habari toka mikoa mbalimbali nchini kushindanishwa.
Hapa kuna inshu ilijitokeza ya kusisimua......
Mwandishi George Nteminyanda akijaribu kuzibaini na kuziainisha aina za bia toka kwenye glasi sita zenye bia tofauti katika shindano la Beer Tasting Competition lililofanyika katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Mwandishi Moses Mathew akijaribu kuzibaini na kuziainisha kwa kuonja na kutizama rangi aina za bia toka kwenye glasi sita zenye bia tofauti katika shindano la Beer Tasting Competition lililofanyika katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Mwandishi Asia Mohamed akionja moja ya glass sita ili kubaini aina ya bia kwenye shindano hilo.
Toka chumba cha Ushindani TBL Mwanza.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya bia TBL Tanzania Doris Malulu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Mabere Makubi wa ITV (kushoto) na Charles Masamba jinsi hatua za uzalishaji zinavyofanyika ndani ya kiwanda cha TBL Mwanza.
Hiki ndicho kinachofanyika.
Uzalishaji ukiendelea kitengo cha uwekaji nembo za bia.
Usafishaji chupa.
Hatua kwa hatua..
Afisa Mahusiano wa kampuni ya bia TBL Tanzania Doris Malulu akitoa ufafanuzi kwa mwandishi wa habari Sitta Tuma.
Kinachotolewa ufafanuzi.
Taswira ya utalii kiwandani TBL Mwanza.
Safari ya utalii kiwandani katika eneo la uzalishaji ilikoma suala lililofuata likawa ni ukabidhi zawadi kwa washindi ambapo picha za washindi unaziona juu kabisa.
Zawadi kwa Philbert Kabago.
Zawadi kwa Mkurugenzi wa Gazeti la Baruti .
Zawadi kwa idara ya usafiri waandishi.
Albert G. Sengo.
Hussein Mtanda.
Sitta Tuma na kwa engo kulia ni uchokozi wa Nteminyanda.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akizungumza na waadnishi wa habari kiwandi eneo la Ilemela jijini Mwanza juu ya hatua mbalimbali za maboresho ya kiwanda na taratibu za kumfikia mteja kwa wakati.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akizungumza na waadnishi wa habari kiwandi eneo la Ilemela jijini Mwanza juu ya hatua mbalimbali za maboresho ya kiwanda na taratibu za kumfikia mteja kwa wakati.
Kutoka kushoto Mbaya, Erick (Afisa Matukio TBL Mwanza), Kabago na  Afisa Mahusiano wa TBL Tanzania Doris Malulu.
Picha ya pamoja ya wanahabari washiriki wa shindano la Beer Tasting Competition 2013-2014 lililofanyika katika kiwanda cha bia TBL Mwanza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.