ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 22, 2013

MMOJA AFA NA WAWILI WAJERUHIWA KWA KUKATWA MAPANGA KANISANI.



Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki na sintofahamu kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi pia ni mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili.
 TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI.
Wadau TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII.
Wadau TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII.
Wananchi wakiwa wakitafakari nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza.
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza .
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.

Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio  hilo na akiiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya uchomaji moto Makanisa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.