ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 17, 2013

WADAU NIKO NJIANI MAMBO YOTE LEO LEO...

Niko eneo la daraja la mto Simiyu wilayani Meatu mkoa mpya wa Simiyu.

Mto huu ambao kipindi cha masika hufurika maji hata kufika kimo cha mita chache kukaribia usawa wa daraja, ukifika majira haya ya kiangazi huwezi amini kwa maji ya mto huu kukauka kabisa ikibakia chemichemi ambayo ndiyo salama kwa wakazi wa maeneo haya linapokuja suala la maji kwa matumizi ya majumbani na kunyweshea mifugo. 

Utekaji maji ukiendelea chini ya daraja kupitia chemichemi usafirishaji nikwa kutumia gari linalokokotwa na ng'ombe.
Kabla ya ujenzi wa daraja hili kipindi cha masika watu waliokuwa wakivuka mtu walikuwa wakifa maji kwa kusombwa na maji hayo sanjari na wengine kuliwa na mamba lakini mara baada ya ujenzi huo kukamilika matukio hayo yametoweka.
Mwanahabari Benedict Kaguo naye yuko nami kwenye tathimini kwenye mto Simiyu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.