Nimesikiliza Hotuba za wabunge wa CCM katika mjadala wa jioni. Wote walikuwa wanajadili wenzao wa upinzani badala ya kujadili vifungu vya Rasimu ya Sheria wanayong'ang'ania kutunga. Nimesikia mipasho na matusi ya Kigwangallah dhidi ya wabunge wa Chadema.
Hadi muda wake unaisha, alikuwa hajachangia lolote kwenye muswada, huku akilaumu wenzake eti wamekataa kufanya kazi yao ya kutunga sheria. Je, yeye ameifanya saa ngapi?
Lililo dhahiri ni kwamba CCM hawataki Katiba Mpya, ndiyo maana wanang'ang'ania mawazo yale yale. Hawana nia njema na mchakato. Ndiyo maana hawataki kusikiliza wenzao.
Bahati mbaya bado wanadhani wananchi wanwasikiliza. Wahenga walinena, sikio la kufa halisikii dawa. Wasubiri matokeo.
Ansbert Ngurumo
Existential Philosopher, Musician, Journalist & Media Manager
Vox Media Centre & Free Media
Tanzania
NAOMBA KUWASILISHA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.