Timu zinazoshiriki michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars zawasili nchini Nigeria
· michuano hiyo inafanyika Lagos, Nigeria kuanzia 16 hadi 22 September 2013.
Timu zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana katika viwajnja vya Agege. michuano hiyo imeudhuriwa na wachezaji guru wakiwemo Rober Pires mchezaji nyota wa zamani wa kablu ya Arsenal
Timu ya Zambia ilikuwa yakwanza kutua siku ya Ijumaa ikifatiwa na timu ya Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. timu ya mabigwa watetezi kutoka Niger ilitua katika uwanja wa ndege wa Murtala Mohammed International siku ya jumamosi mchana pamoja na timu kutoka Congo Brazzaville
kikosi cha timu ya Tanzania kiliwasili siku ya jumapaili chini ya kocha Abel Mtweve na timu nyingine zinategemea kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza siku ya jumatatu
michuano ya Airtel Rising stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa
kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria bwana Segun Ogunsanya
aliongeza "wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote"
michuano ya Airtel Rising stars itafanyika nchini lagos Nigeria kuanzia tarehe 16 hadi 22 septemba 2013. wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika clinic itakayosimamiwa na makocha wa Manchester united inayotegemea kufanyiaka mwaka kesho April 2014 nchini Lubumbashi (Democratic Republic of Congo).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.