ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 18, 2013

TANZANIA YAANZA VIBAYA MASHINDANO YA KIMATAIFA ARS

  • Name of some of the Tanzanian players: Haziz Hashin (keeper), Ramadhan Lida, Petro Joseph, Rothan Mkanwa, Thomas Chindeka, George Emmanuel, Salum Hamisi, Omary Hamisi, Optatus Yustin, Athanas Mdam and Martin Luseke.

  • Mchezaji kiungo wa timu ya Tanzania George Emmanuel akikabiliwa na mchezaji wa timu ya Ghana wakati nchi hizo zilipopambana vikali katika mechi za michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria  Ghana ilishinda 2 - 1

    • mchezaji wa midfield wa timu ya Ghan Michael Owusu akimkabili mchezaji wa timu ya Tanznia wakati timu hizo zilipochuana vikali katika michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja a Onika Lagos Nigeria


Tanzania yaanza vibaya mashindano ya kimataifa ARS
Lagos Nigeria, Jumanne September 17 2013..  Tanzania imeanza vibaya mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya leo kukubali kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Ghana. Mechi ya wasichana inatarajiwa kupigwa baadae leo ambapo watakutana na Sierra-Leone.

Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili, kwa mara ya kwanza yalifanyika nchini Nairobi na Niger kuibuka mabingwa , lengo la mashindano haya ni kuzalisha vipaji vingi vya timu za taifa barani Afrika. 

Katika mechi ya leo , Tanzania ilikua ya kwanza kupata goli katika dakika ya 26 kupitia kwa mshambuliaji hatari Athanas Mdam baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Ghana.

Ghana walifanya shambulizi la hatari na kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa Prince Agyeman baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Tanzania na kuachia shuti kali lilimzidi mlinda mlango wa Tanzania 

Juhudi za Tanzania kupata goli la pili hazikuzaa matunda , dakika ya 45 kipindi cha kwanza Ghana waliongeza bao la kuongoza na lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho kupitia kwa Godfrey Nyarko baada ushirikiano mzuri wa washambuliaji wa Ghana. 

Timu ya wavulana ambayo ipo kwenye  kundi D pamoja na Ghana , Zambia , Sierra-Leone itacheza mechi ya pili dhidi ya Zambia jumatano sembemba 18 , watamaliza na Sierra –Leone katika mchezo wa mwisho wa makundi.

Timu ya wasichana , baada ya kucheza na Sierra –Leone  watakutana na Uganda jumatano , Septemba  18 kabla ya kukutana na Malawi siku ya Alhamisi , September 19. Mashindano yanaingia hatua ya mtoano ijumaa na fainali itapigwa jumapili , Septemba 22.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.