Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiongoza wanachi ktoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Askofu wa EAGT Moses, Kulola |
Mchungaji Kadani Limbu ambaye ni Katibu wa Kanisa la
EAGT Makao Makuu (Ujenzi) akisoma wasifu wa marehemu Askofu Kulola aliyezaliwa
1928 katika Kijiji cha Nyang’honge Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa
kupata elimu ya msingi (Middle School) na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya
mwaka 1946 hadi 1949 kuendelea na masomo na kupata Civil Technician.
Baada ya kumaliza na kupata utaalamu huo na
kuajiliwa kuwa mtumishi wa serikali katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza kama
Mhandisi wa Mchoraji wa Ramani za majengo na Barabara wakati wa uhai wake
aliamua kuacha kazi na kuanza utumishi wa mungu akifanya kazi kwa kutembea kila
mahali akihubiri Injili kwa watu mbalimbali.
Wasifu huo ulimwelezea Askofu Kulola wakati wa
utumishi wake wa kiroho alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia mwaka 1962 baada ya
kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na matatizo na kuwahi kufungwa gerezani
na kupigwa na bwana jela na kuumizwa vibaya muguu wake wa kushoto na kupelekea
kupata kilema na kuwekewa mguu wa bandia.
Marehemu Askofu Kulola ameacha mke na watoto 10
wajukuu 42 vitukuu 16 na amekuwa mutumishi wa kiroho kwa kuanzia akiwa na umri
wa miaka 18 na jana amezihilisha kutokana na umati mkubwa uliofika kumuaga
kwenye uwanja wa michezo wa kirumba Jijini Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.