ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 19, 2013

AIRTEL YAKABIDHI FUNGUO YA NYUMBA YA KWANZA IRINGA


Madereva  wa  boda  boda  mjini  Iringa  wakitoka maeneo ya  Frelimo mjini  Iringa wakati wa  ziara  ya wafanyakazi  wa Airtel makao  makuu na Iringa  kumtembelea mshindi  wa  nyumba  ya  kwanza  ya Airtel Yatosha  Bw Sylivanus Juma Wanga  ambae  ni mhasibu wa taasisi  isiyo ya  kiserikali ya TARWOC ambae amekabidhiwa funguo ya nyumba  yake  na kuelekea  jijini Dar es Salaam kukabidhiwa nyumba yake mwishoni mwa wiki hii

Meneja  wa Airtel mikoa ya  kusini Beda Kinunda  akimkabidhi funguo ya nyumba mshindi wa  nyumba ya kwanza  ya Airtel Yatosha  jana  kutoka Frelim mjini Iringa Bw Sylivanus Juma Wanga  wanaoshuhudia  ni mke wa mshindi Bi Veronica  Wanga na Meneja  uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando
Picha  namba  10

Mshindi  wa nyumba  ya kwanza  ya Airtel Bw Sylivanus Juma Wanga   na ndugu  zake wakifurahia  kutembelewa na  wafanyakazi  wa kampuni ya simu ya Airtel nyumbani kwao Frelimo mjini Iringa kwa  ajili ya kukabidhiwa funguo na hati ya  nyumba  yao kabla  ya kuelekea  Dar es Salaam kukabidhiwa funguo za Nyumba yake  kulia wa kwanza ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando, meneja  wa  Airtel nyanda za juu kusini Beda Kinunda ,mke  wa mshindi Bi Veronica Wanga ,Bw Sylivanus Wanga na shemeji  yake Bi Martha Kibiki

Meneja  uhusiano wa Airtel Bw  Jackson Mmbando  akimkabidhi cheti cha ushindi wa nyumba ya kwanza ya promosheni ya  Airtel yatosha Bw Sylivanus Juma Wanga   ambae ni mkazi  wa Frelimo Iringa katikati ni mke wa mshindi  huyo Bi Veronica Wanga.

Hii  ndio  nyumba anayoishi mshindi  wa nyumba ya kwanza ya Airtel yatosha Bw Sylivanus Juma Wanga   iliyopo  eneo la Frelimo mjini Iringa

Mshindi wa nyumba Airtel, akabidhiwa funguo  Iringa.
      Kusafirishwa na Airtel kuja dar alhamisi wiki hii kupokea nyumba yake
Hatimaye mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha yenye thamani ya shilingi milioni 65/- iliyotolewa na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel, mwishoni mwa wiki hii amekabidhiwa rasmi funguo yake baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel yatosha shinda nyumba 3.

Makabidhiano ya funguo hiyo kwa mshindi, Bw. Silvanus Juma yalifanyika mwishoni mwa wiki hii mkoani Iringa na kushuhudia mshindi huyo wa Airtel akikabidhiwa funguo pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema “ makabidhiano ya hizi funguo ni ya awali lakini Alhamisi ya wiki hii mshindi huyu Bw. Silvanus Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam” Aliendelea kwa kusema Airtel inayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wao huyo zawadi hiyo na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja wake nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali inazoendeshwa na Kampuni hiyo.

“Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya ya Airtel yatosha shinda nyumba 3. mbalimbali za Airtel ili kushinda,” alisema Mmbando.

 Aliongeza Mmbando kwamba ili mteja wa Airtel aweze kujiunga na vifurushi hivyo anapaswa kupiga *149*99# na kuchagua 1 au 2 kisha aweze kujiunga na kifurushi chochote cha wiki, siku au mwenzi hiyo ndo njia pekee ya kushinda.

Mpaka sasa  Airtel imeweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake nchi nzima ambapo imetoa shilingi milioni 37  kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90, sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni bado zinashindaniwa kupitia promosheni hiyo ya Airtel yatosha, shindanyumba 3.

Akielezea furaha yake Bw. Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali na hata alipopigiwa simu hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani na hawezi kupata nyumba katika msimu kama huo.

“Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini. Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo wazi kuwa Airtel ni mtandao unaojali na kuthamini wateja wake,” alisema Juma.

Bw Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu ilyopelekea Bw. Juma kuibuka mshindi wa kwanza katika promosheni hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.