ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 15, 2013

MH. MAKAMBA NA MH. KABWE WAHUDHURIA SHOW YA KIJANJA YA MWANA FA 'THE FINEST' NDANI YA UKUMBI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA.

IMG_7288
Mwana FA akiwasili katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam huku akiwa amevalia suti matata iliyotengenezwa na mbunifu wa mavazi anayekuja kwa kasi nchini Sheria Ngowi.(Picha zote na Geofrey Mwakibete wa Mo Blog).
IMG_7336
IMG_7422
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akikamua jukwaani wakati wa Show ya Kijanja ya The Finest iliyorindima usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar. Nyuma yake ni Msanii Linah aliyeshirikishwa kwenye nyimbo ya YALAITI aliyoimba na Mwana FA akisubiri kutumbuiza.
IMG_7361
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Ben Paul akisindikiza kutoa burudani wakati wa show ya Mwana FA iliyopewa jina la “The Finest”. Wasanii wote walionekana nadhifu kwa kuvaa masuti ya gharama.
IMG_7357
Kutoka (kulia) ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa Bumbuli (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald Hando.
IMG_7427
Mashabiki wa Mwana FA, wakimshangilia Superstar wao wakati akitoa burudani.
IMG_7430
Mrembo wa Wema Sepetu na Kidate wake nao walikuwepo kwenye show ya wajanja.
Fa 7
Mashabi wa Mwana FA wakionekana kukongwa mioyo yao wakati wa show iliyobeba jina la  “THE FINEST”…Na kweli ilikuwa The Finest kama inavyoonekana pichani.
IMG_7330
Watu weweeeeeeeeeee…..ukumbi ulirindima Shangwe za mashabiki wa Mwana FA.
IMG_7418
Mwana FA akiendelea kuwapa raha mashabiki wake.

Asma Makau, Jojo, Shadee & Afriend wakiwa nje ya ukumbi wa makumbusho ya Taifa Dar es salaam kwaajili ya kuingia ndani kushuhudia 'The Finest'. 


Vanessa Mdee na B Dozen katika viwanja vya Makumbusho kabla ya 'The Finest' Show 

IMG_7399

Wadau wakishow love nje ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Halima Kambi, Dar.
KATIKA Shoo hiyo ya ‘Kijanja’ pia ilihudhuriwa na wasomi kibao huku baadhi ya wabunge kama Mh. Zitto Kabwe na January Makamba wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wajanja waliohudhuria katika shoo hiyo ya “kijanja” ya ‘The Finest’ iliyofanyika  katika Ukumbi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Mwana FA, pia alisindikizwa na na baadhi ya wasanii kama, Ben Paul, Linah, Maua, Dully Sykes na wengine kibao pamoja na bendi ya Njenje.

Show ilifana sana kutokana na utaratibu na mpangilio na maandalizi ya shoo yenyewe na MwanaFA aliweza kufanya yake jukwaani na kuwapagawisha mashabiki wake katika usiku ule.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. mbona hamjaongelea idadi ya watu waliohudhulia?...shame on you guyz, jamaa hatarudia tena kupambana na Jide...na nyie msiwe mnamdanganya mnampoteza mwenzenu, by the way watu nw washachoka kuibiwa!

    ReplyDelete
  2. Mbona hamjaiongelea na kuilinganisha show ya mwanaFA na ya Jide? shame on you guys! Clouds mmeonyesha ubovu wenu na bias yenu, watu walivyosema mwanaFA anatumiwa na Ruge sikuamini, ila kwa jinsi ilivyoonyesha ktk hili nimeamini kweli clouds mafisadi na naamini anachokisema Ladyjaydee!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.