Mabondia wanne wa Tanzania wafungwa miaka 15 jela nchini Mauritius kwa makosa ya kuingiza dawa za kulevya aina ya heroin.
Mabondia waliohukumiwa |
Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa, wote walikiri makosa ya
kuingiza mihadarati hiyo nchini Mauritius wakati walipokwenda kushiriki
mashindano ya ndondi barani Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji,
waliiambia mahakama kuwa walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu
kutokana na hali zao za maisha kuwa maskini.
"Tunaomba radhi kwa
taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na
tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi
tungepata kiasi cha Pauni £4,000". Walisema
Jaji Benjamin Marie
Joseph alisema katika kutoa adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa
ushirikiano mzuri wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata
wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa
siku 1,722, sawa na miaka miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia
jela. Pia watatakiwa kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za
uendeshaji wa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa mwandishi
wa habari wa BBC nchini Mauritius Yasine Mohabuth in Mauritius, Jaji
aliwashutumu kwa kuukosea umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya
aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili
Mauritius tarehe 10 Juni 2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa
hadi walipokamatwa katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram
4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
CHANZO/bbc swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.