ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 8, 2013

WASANII WA KIZAZI KIPYA WANG'ARISHA TAMASHA LA AIRTEL YATOSHA MBAGALA

Msanii mahiri wa Hi Hop nchini maarufu kama FID Q akikamua katika jukwaa maalum la kuitambulisha huduma kabambe ya Airtel Yatosha katika viwanja vya Zakhem jiini Dar es Salaam na kufanikisha kuwaunganisha watanzania na wakazi wa jijini Dar es salaam kwenye huduma ya Airtel Yatosha.


Wasanii wa kundi la Wanaume Halisi wenye makazi yao Jijini Dar es salaam Temeke wakitoa Burudani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu

Mwanadada msanii chipukizi wa temeke akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vya zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii

Msanii wa kikundi cha tip top connection Madii akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vy zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii

Kikundi cha wakali dansi cha temeke kikitoa burdani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu.

Maneno kuntuu' toka kwa wanaume halisi.


Wasanii wa kizazi kipya wangarisha tamasha la Airtel yatosha Mbagala

Burudani ya tamasha la Airtel yatosha katika viwanja vya mbagala zhakem katika siku ya jumamosi na Jumapili zilifana kwa kupambwa na burudani kibao toka kwa wasanii wa kizazi kipya wakiwemo kundi zima la wanaume halisi likiongozwa na sir juma Nature, kiongzi wa tip top connectionMadii, kundi la wakali wa dansi pamoja na wasanii mbalimbali wakiwemo Ney wamitego na Roma Mkatoliki

Akizungumzia juu ya tamasha hilo Meneja Uhusiano wa Airtel bwana Jacksoni Mmbando alisema" tumeweza kushuhudia burdani kabambe kutoka kwa vikundi mbalimbali vya wasanii wa kizazi kipya na wasanii chipukizi wa temeke katika viwanja vya zhakem Mbagala.  lakini pia mbali na  burdani wateja wa Airtel wameweza kuunganishwa na huduma ya Airtel yatosha na kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na faida zake, wateja waliweza kujiunga na kusajili namba zao”.

"Tunawashukuru watanzania na wateja wetu wote waliojitokeza kwa wingi kupata burdani hii na tunawahaidi kuendelea kuwapa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kutanua wigo wa mawasiliano nchini aliongeza "Mmbando

huduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha  mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama poa ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.pamoja muda wa maongezi mteja anapata vifurushi vya kutuma ujumbe mfupi na internet na vifurushi hivi vinapatikana kwa siku au kwa wiki, ili kujiunga na huduma hiipiga *149*99# ufurahie huduma poa na ujionee "Airtel Yatosha"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.