ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 29, 2013

AIRTEL YAZINDUA MICHUANO YA AIRTEL Rising Stars 2013

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo , wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo(katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu

Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo akikazija jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye halfa ya uzinduzi wa program ya Airtel 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni

Wakizindua program ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2013

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012


Airtel yazindua michuano ya Airtel Rising Stars 2013

Dar es Salaam, Jumanne 28 Mei 2013… Airtel Tanzania leo imezindua michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Airtel imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kudhamini mashindano hayo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na serikali kukuza vipaji vya soka nchini Tanzania.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo tangu kampuni ya airtel ianze kudhamini mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo huanzia ngazi ya mkoa hadi Taifa. Fainali za Airtel Rising Stars Taifa hufatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa kwa wachezaji nyota chini ya ukufunzi wa makocha mahili wa vijana kutoka klabu ya Manchester United.

“Nafurahi kwamba tumepiga hatua na leo tunazindua msimu wa tatu wa Airtel Rising Stars ambao bila shaka utakuwa wa ushindani na wa kusisimua”, alisema Beatrice Singano, Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya Airtel Tanzania. Uzindinduzi huo ulifanyika katika ofisi za TFF.

Singano alisema: “Airtel imevutiwa na mwitikio wa vijana wengi waliojitokeza kujiandisha na kushiriki katika mashindano ya Airtel Rising Stars katika miaka iliyopita. Ni matumaini yetu kwamba vijana wengi zaidi watajitokeza kushiriki mwaka huu”.

Singano alisema mpango huu kabambe unawalenga wasichana na wavulana nchi nzima ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa mawakala wa soka, makocha na mamlaka nyingine zinazohusika na programu za kuendeleza vipaji vya soka. Mwaka huu Airtel Rising Stars itajumuisha jumla ya timu 24 za wasichana na wavulana kutoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Morogoro, Ilala, Kinondoni Temeke, Kigoma, Tanga na Ruvuma ambao baadhi yao watateuliwa kuunda timu za mikoa yao katika fainali za Taifa. Vile vile mashindano ya Taifa yatatumika kuteua timu itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa (inter-country tournament)

Akizunguma katika hafla hiyo, mgeni rasmi Mkurugezi wa Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na Airtel kuwekeza kwenye programu ya soka ya vijana ambao ndiyo nguzo mhimu kwa maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Kauli yake iliungwa mkono na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF Bw Basibu Ramadhani ambaye alisema program za soka za vijana ndio njia pekee ya kuinua kiwango cha soka nchini.

“Tumeshudia vipaji vingi katika mashindano yaliyopita na bila shaka michuano ya mwaka huu yataendelea kutoa vipaji vingine vingi. Natowa wito kwa timu kubwa hapa nchini kutumia fursa hii kupata wachezaji chipukizi kwa ajili kuimarisha timu zao. Nawatakia washiriki wote mashindano mema na wazingatie nidhamu na taratibu ya mchezo wa soka.” alisema Thadeo.

Programu hii ya Afrika inaungwa mkono na klabu kubwa ya Manchester United kwa lengo la kubaini vipaji vya soka na kuviendeleza ili kuweza kuonekana kwa mawakala, makocha na kupata nafasi ya kutambulika kitaifa na kimataifa.
Ushirikiano wa Airtel na Manchester United katika kuendeleza soka ya vijana ni utekelizaji wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya pande hizo mbili mwezi Disemba 2010 ambayo yanaiwezesha Airtel kutumia hazina ya ufundi wa soka kutoka klabu hiyo kubwa duniani kuendeleza vijana chipukizi barani Afrika.

Vijana wanaoshiriki Airtel Rising Stars mwaka huu hapa nchini wanatajiwa kuanza kujiandikisha mwezi ujao na jumla ya timu 24 kutoka mikoa 9 zitashiriki. 

Airtel ni kampuni ya simu za mikononi inayofanya biashara barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Democratic Republic of Congo, Gabon, Ghana, Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda, na Zambia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.