ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 22, 2013

UJIO WA WADAU WA MAENDELEO JIJINI MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa Akitoa Salam za Mkoa kwa Wageni hao.


Kiongozi wa Ujio huo Bw. Alberic Kacou. Akitoa salam za Ujumbe huo.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi Dorothy Mwanyika akitoa Neno la Utangulizi kwa Wageni hao.

Mtaalam kutoka Wizara ya Fedha akifafanua Jambo katika kikao cha Pamoja.

Bara bara ya Mawe kama Inavyo Onekana katika Eneo la Igogo Jiji Mwanza.
Leo kubwa katika Mkoa wa Mwanza tumepokea Ugeni wa Wadau wa mashirika ya Maendeleo kutoka (DPG), Ambalo linajumuisha balozi zote zilizopo hapa nchini, Zikiwapo Jumuiya ya Ulaya,Wakuu wa Mashirika ya Ufadhili, wa Maendeleo kama NDP, WB, AFDB, JICA UNICEF.
 
Ujumbe huu umefika Mkoani hapa na Kuonana na Vingozi wa Mkoa wa Mwanza, akiwapo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watendaji wengine wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Wataalam wengine wa taasisi za umma zilizopo katika  Mkoa huu.

 Katika ziara yao hiyo, wamepata kusikia Speach kuhusu Masuala Mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huu. Lengo la Ziara Hiyo ilikuwa Kutembelea na kuona jinsi Miradi mbalimbali ya maendeleo inavyo tekelezwa, hivyo wametembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa huu ikiwapo,  Mradi wa barabara za Mawe, unao tekelezwa katika Mkoa huu hususan katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

 Hata hivyo kwa mujibu wa ratiba yao siku tarehe 23/4/2013, watafanya ziara katika Mkoa wa Geita.

Kuhusu mambo mengine Mwanza ni salama, Mvua zipo za wastani, na jua linawaka kwa Mbali.

Karibuni sana kwa ajili ya Kula Samaki watamu wa ziwa Victoria namaanisha Sato na Sangara bila kuwasahau Mumi...weeee!!!.
 
Na:  Atley  Kuni Mwanza - Afisa habari Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.