Ibrahimu Class 'King Class Mawe akioneshana ujuzi wa kutupiana makonde na Shabani Mhamila 'Star Boy' |
Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com |
Na MWANDISHI WETU
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya
|
kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa kumchakaza Jibaba ili kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali" alisema Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga Theodor Luanda Frebruary 2,1996 na kutetea vema
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila,Japhet Kaseba,Hassani Matumla,Rashidi Matumla dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis Miyeyusho, Said Mundi na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' pamoja na mabondia mabingwa wa dunia
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.