Makabu (kulia) na Gogito (kushoto) |
Yale mapambano mawili ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu kubwa sana katika bara la Afrika yamefanyika katika majiji mawili ya Johennsburg, Afrika ya Kusini na Tunis, Tunisia baada ya kuibuka miamba miwili katima ubingwa na uzito tofauti!
Katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Mkongo man Ilunga Makabu alimchakaza bila huruma bondia Gogito Gorgiladze kutoka nchini Georgia kwa TKO katika raundi ya nne (4)!
Mawili hao walikuwa wanagombea ubingwa wa dunia wa vijana walio chini ya miaka 25 katika uzito wa Cruiserweight na mpambano huo ulirushwa moja kwa moja na televisheni ya Super Sport!
Mambo yalianza kujionyesha katika raundi ya kwanza tu wakati bondia Makabu alipokuwa anarusha ngumi ya mkono wa kushoto ambayo ilikuwa inafanya madhara yasiyojificha kwa Gogito!
Katika raundi ya pili na ya tatu Gogito alikuwa anarudi nyuma na kuongea kana kwamba anamwambia Illunga asimwadhiri mbele ya watu lakini Mkongo man Makabu alisonga mbele akirusha makonde mazito bila huruma. Ilipoanza raundi ya nne (4) Ilunga alirusha makonde sita ya kasi ambayo yalimfanya referee wa mpambano huo Wally Snowball wa Afrika ya Kusini kuingialia kati na kusimamisha mpambano huo!
Golden Gloves ya Rodney Berman ndiyo iliyoandaa mpambano huo na Illunga amepangwa kuteta taji lake mwezi ujao nchini Monaco katika tamasha la “The Last Man Standing” litakalofanyika katika jiji la Monte Carlo!
Waamuzi wa mpambano huo wakiongozwa na Rais wa IBF Africa MtanzaniaOnesmo Ngowi aliyekaa katikati. |
Nchini Tunisia, bondia anyeishi nchini Belgium, Ayoub Nefzi aliidhihirishai nchi ya Tunisia kuwa yeye ndiye mtu pekee atakayeipeleka katika nafasi nzuri ya ngumi duniani baada ya kumchakaza vibaya bondia Ishmael Tetteh wa Ghana katika raundi ya 7.
Mpambano huo uliofanyika katika jiji la Tunis uliwavutia mashabili wengi wa nguni kutoka katika nchi za Afrika ya Magharibi na Kaskazini ambao walifurika jijini Tunis kuuangalia.
Mpambano huo ulikuwa wa kugombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Jr. Middle na uliandaliwa na Halmashauri ya jiji la Tunis katika juhudi zake za kukuza 'Utalii wa Michezo" (Sports Tourism).
Ayoub Nefzi atakuwa kwenye kindumbwendubwe kingine nchini Belgium mwezi wa tatu (March) kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara (IBF Intercontinental Title) hivyo mpambano wake na Ishmael Tetteh ulikuwa kama wa maandalizi wake.
Hii ni mara ya kwanza kwa IBF kufanya shughuli zake katika nchi ya Tunisia kutokana na nchi hiyo kuegemea katika mashirikisho mengine ya ngumi!
IBF sasa inachukua nafasi ya katikati katika ngumi barani Afrika na hii inaleta hamasa kubwa kwa mashabiki wengi wa ngumi!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.