ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 19, 2013

KANISA JINGINE LANUSURIKA KUTEKETEZWA ZANZIBAR

Taarifa kutoka Zanzibar za muda mfupi uliopiata kwa mujibu wa ITV zimesema kuwa kanisa la Shalom Ministry lililoko mkoani Kusini Unguja limenusurika kuteketea kwa moto mara baada ya watu watatu wasiojulikana kuvamia eneo la kanisa hilo majira ya saa 9:30 usiku wa kuamkia leo kisha kumteka mlinzi na kumshambulia.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kusini Unguja, Agustino Ulomi amesema kuwa   ili kuokoa uhai wake mlinzi huyo mara baada ya kuzidiwa nguvu alitafuta upenyo na kuwakimbia wavamizi hao kitendo kilichowapa mwanya kuingia ndani ya kanisa hilo na kukusanya viti na kuvitia moto kisha wakatokomea kusiko julikana.

Akishuhudia kwa kificho hali hiyo mlinzi wa kanisa hilo alitoa taarifa kwa jeshi la polisi na kupata msaada ulio wahisha juhudi za kuzima moto huo. 
Zaidi Sikiliza sehemu ya SAUTI ya Taarifa iliyoruka ITV.

Juhudi zinaendelea kubaini wahusika wa tukio hilo ikiwa ni ulinzi kuimarishwa. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.