Katika hali
isiyokuwa ya kawaida kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa soko kuu la jijini
Mwanza leo amezuwa sokomoko na taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo mara
baada ya kukutwa na jeneza la kusafirishia maiti katika sehemu yake ya biashara
tena juu ya magunia ya viazi sokoni hapo.
Aliyezua
taharuki hilo ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza
ambaye pia ni mfanyabiashara wa viazi wa soko hilo Bw. Hamad Nchola ambaye
alikuwa hakuwa na majibu ya moja kwa moja balimajibu mafupi mafupi
yasiyoridhisha wakati akihojiwa na waandishi wa habari.
Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakijadiliana juu ya kuwepo kwa jeneza hilo katika eneo la banda la biashara la mwenyekiti soko kuu la Mwanza.
Jeneza juu ya magunia ya viazi ndani ya banda la biashara la mwenyekiti.
Bw. Hamad Nchola ambaye ni mwenyekiti wa wafanyabiashara soko kuu la Mwanza aliyezua balaa.
Naye
Mwenyekiti huyo akijitetea kuhusu sakata hilo amesema kuwa aliamua kufanya
uamuzi huo wa kuhifadhi jeneza hilo sokoni hapo kwenye sehemu yake ya biashara
mara baada ya kulichukuwa kutoka msikitini akisubiri usafiri kulipeleka
hospitali ya Rufaa ya Bugando kuuchukuwa mwili wa mke wa mfanyabiashara
mwenzake sokoni hapo ambao ulipaswa kusafirishwa kuelekea wilayani Magu kwa
mazishi. Msikilize kwa kubofya play.
Alipohojiwa
kwa nini asingeliacha jeneza hilo msikitini au kulipeleka nyumbani
kusubiri muda muafaka badala ya kulihifadhi
sokoni hapo ambako kunatambulika kuwa ni sehemu mahususi kwaajili ya biashara ya
mazao na chakula pamoja na kuwa na watu wenye imani tofauti, mfanyabiashara
huyo alisema aliamua kufanya hivyo kwakuwa hakuona shida na alifanya hivyo kama
wafanyabiasha wengine na kwamba inshu hiyo imekuwa kubwa kwa kuwa yeye ni
kiongozi.
Kisha
akaongeza kuwa kufanya hivyo siyo tatizo na jeneza hilo ni mbao tu na siyo kitu
cha kustaajabisha na aliamua kulihifadhi eneo la biashara yake kwa kuhofia kuwa
lingenyeshewa na mvua.
Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakichungulia eneo la banda la biashara la mwenyekiti ambapo kuna jeneza hilo.
Pamoja na
kuwa na kigugumizi kujibu kuhusu muda alilolileta jeneza hilo sokoni hapo
kwamujibu wa mmoja wa walinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa
jeneza hilo liliingia sokoni hapo mapema alfajiri wakati hakukuwa na wafanyabiashara
sokoni hapo hali ambayo ilimshitua na mlinzi huyo akashindwa kuhoji kwakuwa ni
mfanyabisha huyo ni bosi wake.
Mmoja kati ya wafanyabiashara akiwasilisha maoni yakekuhusu tukio hilo.
Hata hivyo
baadhi ya wafanyabiashara waislamu wamepinga vikali kuwa jeneza hilo si mali ya misikiti kwa
kuwa waumini hao hawatumii masanduku ya miundo hiyo hususani hilo lenye tundu la kuagia, zaidi ya kutumia majeneza
yenye mikono minne hivyo wamemtaka kiongozi huyo kuhojiwa zaidi juu ya sakata
hilo. Sikiliza kauli za wafanyabiashara...
Mmoja kati ya wafanyabiashara akiwasilisha maoni yakekuhusu tukio hilo.
Vijana wakifanya mchakato kuliondoa jeneza hilo sokoni hapo toka kwenye banda la biashara la mwenyekiti.
Hatimaye Jeneza
hilo liliondoshwa sokoni hapo na vijana waliolibeba msobemsobe kwenye majira ya
saa 4 asubuhi ya leo lisijulikane lilipoelekea.
Mwendo msobemsobe.
Mwendo msobemsobe sasa ni kuelekea lango kuu.
Sakata hilo limezua maswali mengi kwa wadau wa biashara jijini hapa huku likihusishwa na masuala ya kishirikina na U-freemanson.
WAZIRI KOMBO AAGANA NA BALOZI WA IRAN
-
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Mahmoud Thabit Kombo ameagana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Mhe.
Hossein Al...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.