Azam
FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Khalfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh
katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu
ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.
El-Mereik
wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho
Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha
mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo
vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.
Kuuzwa
kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha
zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha
kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati
Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka
lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi
milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye
kufikia dau hilo waweze kumuuza.
Mengi
yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa
Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh
kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa.
Mrisho
Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda
nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati baada ya TP Mazembe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.