Rais JK akiwa na meneja wa Wings of Kilimanjaro
jijini Arusha.
|
Wings of Kilimanjaro, tukio linalotokea mara moja katika maisha inategemea kufanyika mwishoni mwa Januari 2013, itategemea kupata kiasi cha watu 200, watalaamu wa spoti inayoitwa ‘paragliding’ and ‘philanthropists’ wakitembea mpaka kilele cha Mount Kilimanjaro kwa kupaa kilele ya Afrika.
Kwa kufanya hivi, nia ya tukio hili nikupata dola million moja ambayo itasaidia taasisi tatu ambazo zinafanya kazi yakusaidia jamii hapa Tanzania, ni ‘Plant With Purpose’, ‘One Foundation’ na ‘World Serve International’.
Katika siku ya uzinduzi, wataalamu wa paragliding (ikiwemo wale amabyo wanajulikana duniani) na abiria wao watazindua siku hiyo na kwenda eneo la Moshi ambapo watatua. Muda wa kuruka angani mpaka Moshi itatumia dakika 40.
Mapema wiki iliyopita, Meneja wa Wings of Kilimanjaro, Bi Paula McRae alipata nafasi yakukutana na Mhe. Raisi Jakaya Mrisho Kikwete katika safari yake huko Arusha. Alipokuwa anaongea naye kuhusu tukio la Wings of Kilimanjaro, raisi alifurahi sana na aliwashukuru kwa timu ya Wings of Kilimanjaro kwa kutoa ushirikiano kwa njia ya juhudi ya kutafuta fedha na pia kuweza kupromote Mt. Kilimanjaro ulimwenguni.
Raisi aliendelea kutambua habari katika vyombo vya habari ikizugumzia boti ya Mt. Kilimanjaro ambayo ilikuepo London, nchini Uingereza (zaidi ya watu milioni 20 wanaangalia katika kipindi cha BBC), pia iliweza kutoka kwenye magazine ya National Geographic na pia kupokelewa na balozi wa hiari, Doug Pitt.
Timu ya Wings of Kilimanjaro wanafurahia kuwaonyesha wa Tanzania mchezo ambao haijulikani sana nchini, inayoitwa ‘paragliding. Timu ya Wings of Kilimanjaro itatoa ushindani tukikaribia katika tukio, wa Tanzania wawili wataweza kusafiri na rubani wa paragliding mwezi wa pili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.