ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 5, 2012

KANISA LA MOROVIAN NYAKATO JIJINI MWANZA LAKATAA MISAADA KWA SHARTI WALILOPEWA LA KURUHUSU USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA


Kanisa la Morovian Nyakato jijini Mwanza limesema katu halitofungua milango kwa wahisani na wafadhili wanao shinikiza kanisa hilo kuruhusu ndoa za jinsia moja na suala la ushoga kama moja ya masharti ya kupata misaada.

Hilo limebainishwa jana na Mchungaji wa kanisa la Morovian lililoko Nyakato jijini Mwanza Mch. Ezekiel Yona, wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa ni moja kati ya changamoto kwa kanisa lake lilizokumbana nazo wakati wa kufanikisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum ili kuiweka jamii pamoja na kutambua kukua kwa lindi la watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu linalohitaji kiasi cha shilingi milioni 43,050,000/= kukamilika.


Mch. Ezekiel amesema kuwa jengo wanalolimiliki sasa limejengwa kwa michango ya waumini wazalendo waliojitolea baada ya kukataa misaada ya mashirika ya nchi fulani (majina ameyahifadhi) ambayo yalitoa masharti kwa kanisa hilo kukubali kuwa na ndoa ya jinsia moja  ambayo ni nje ya maadili ya jamii ya watanzania na kanisa la Mungu, hivyo wameamua kuuthibitishia ulimwengu kuwa kanisa la Mungu litajengwa na washirika wenyewe.

Bofya play..


Mnamo jumapili ya tarehe 9 mwezi huu disemba 2012 Kanisa la Morovian Nyakato litaendesha harambee kuchangia kumalizia ujenzi walioanza hivyo kamati ya ujenzi wa kituo hicho wamewaomba wanajamii kushiriki katika jambo hilo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi mbalimbali wameahidi kuhudhuria.


Ni majengo ya kituo hicho cha kanisa Morovian nyakato jijini Mwanza kilichojengwa na wananchi waumini wenyewe.


Kuhusu suala la baadhi ya vituo kuanzishwa kwa maslahi ya wamiliki wa vituo hivyo binafsi mjumbe wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha kanisa Morovian Nyakato ametoa wito kwa serikali kuunda chombo kitakacho kupitia mfumo wa uendeshaji wa asasi hizo hivyo kulea watoto kubaini mapungufu ikiwa ni pamoja na kuvifungia na kuvifuta vituo vyenye sifa zisizo stahili. Kumsikiliza Bofya play..

Moja kati ya changamoto inayolikabili kanisa hilo ni Dampo la takataka lililo katikati ya barabara ambalo mpaka sasa takribani wiki kadhaa linajaa takataka bila kuzolewa utadhani serikali ya wilaya haipo na limekuwa kero kwa kwa harufu na hatari kwa afya ya  jamii iishiyo mazingira hayo.

Mfereji usio rasmi unachuruzisha maji yenye mafutamafuta yenye harufu kali toka kwenye dampo lililopo eneo hilo tena katikati ya barabara kuifanya kuwa ngumu kupitika. 

Ni mfereji wenye mazalia ya funza (kama wanavyoonekana pichani) na wadudu wengine hatari kwa afya ya wakazi wa eneo hili.

Halmashauri ya jiji la Mwanza kitengo cha Afya mnayaona haya?
Hamjawahi fika eneo hili hatarishi kwa afya?
Yasemekana mnazo taarifa, Je masikio mmetia pamba au?

Pembeni nyumba ya ibada pembeni kituo kwa cha kulelea watoto wa mitaani, watoto yatima na waishio katika mazingira magumu, tazama eneo hili na mazingira ni kama hayo.

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.