TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
OCTOBA 22, 2012
Leo hii nilituma taarifa ambayo ilijaribu
kuijibu makala iliyoandikwa na "Imani Makongoro" mwandishi
mwandamizi wa gazeti la Mwananchi. Taarifa hiyo ya Makongoro iliyokuwa na
kichwa cha habari “Umbumbumbu wa Imani Makongoro mwandishi wa gazeti la
Mwananchi” ilitumwa kwenye vyombo vya habari leo hii!
Nataka kuchukua fursa hii kuifuta
taarifa hiyo na kuwaomba radhi Imani Makongoro, gazeti la Mwananchi pamoja na
wasomaji wote walioipata na kusumbuliwa na taarifa hiyo!
Nafanya hivi nikijua kuwa taarifa
yenyewe ilitoka kabla ya kushauriana na washauri wangu. Naamini kuwa
uandishi wa habari ni wito na unafanyika katika mazingira magumu sana hapa
Tanzania.
Mimi sina nia ya kuisema wala
kuikandamiza taaaluma ya uandishi wa habari. Aidha sina haja ya kuwafanya
waandishi wa habari wasiandike yale wanayofikiri kuwa ni mema kwa jamii!
Ndiyo maana nachukua fursa hii
kumuomba radhi Imani Makongoro, Gazeti la Mwananchi pamoja na wote waliopata
taarifa ile kwa usumbufu walioupata.
SAMAHANINI SANA!!!
Imeandikwa na:
Onesmo Ngowi
Rais wa,TPBC, IBF AMEAPG, ECAPBA
Mkurugenzi CBC
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.