Meneja wa NMB Tawi la Songea Rehema Nasibu akikabidhi madawati kwa Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Songea Vicent Kayombo. |
Benki ya NMB kanda ya kusini imetoa msaaada wa madawati themenini yenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule nne za msingi wilayani songea ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule mbalimbali wilayani songea.
Msaada huo wa madawati unatarajia kupunguza upungufu wa madawati katika wilaya hiyo kwasasa wilaya inaupungufu wa madawati elfu mbili mianne na themanini .
Benki ya NMB imetoa madawati hayo kwa shule nne za msingi wilayani hapa ambazo ni shule ya msingi Ifugwa,Sokoine ,Inuka twende na shule ya msingi Bwabwasi, meneja wa banki hiyo kaanda ya kusini THOMAS KILANGO amesema kwakuwa benki hiyo inafanya kazi na wanajamii hivyo ni wajibu wao kushirikiana naserikali kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
Aidha msaada huo wa madawati katika wilaya hii ya songea umepunguza changamoto ya upungufu wa madawati kwakuwa wilaya ilikuwa na mahitaji ya madawati 2,480 mianne na themaninina baada ya msaada huo mahitaji ya madawati ni elfu mbili na mianne, VICENT KAYOMBO kaimu mkurugenzi wa wilaya ya songea amesema wilaya inamadawati elfu kumi 10,313 kati ya madawati 13,113
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.