ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 23, 2012

HATIMAYE MBUNGE WA ILEMELA AFANIKIWA KUSITISHA MGOMO WA EXPRESS ZA KILIMAHEWA

Ule mgomo wa daladala za jijini Mwanza maarufu kama Express za njia ya Ilemela - Kiloleli hatimaye leo umekoma mara baada ya mbunge wa Ilemela Highness Kiwia kuwakutanisha wawakilishi wa vyombo hivyo vya usafiri pamoja na mkandarasi na hatimaye kupata muafaka.

Njia mbadala.

Kulikuwa hakuna njia mbadala na vyombo vya usafiri vikikomea eneo la Big Bite hiyo ni mara baada ya kukatwa kwa daraja la eneo la Big Bite, ili kupisha ujenzi wa daraja jipya lenye uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya maji yatiririkayo kutoka maeneo ya juu milimani ambayo mara zote yamekuwa yakileta dhahama kwa wakazi waishio maeneo hayo sambamba na kuharibu miundombinu ya barabara vipindi vya mvua.
Mbunge huyo wa Ilemela kupitia CHADEMA alimpiga mkwara mzito mkandarasi huyo kwamba ni suala la kustaajabisha kwa mkandarasi aliyepewa dhamana na jiji kwa uaminifu, kujenga daraja hilo kiungo muhimu bila kuunda njia mbadala kuwezesha vyombo vya usafiri kupita.

Hii leo njia mbadala imeanza kutengenezwa ili kuwezesha vyombo vya usafiri kufanya safari zake kwa urahisi tofauti na njia finyu iliyobuniwa kupitia barabara nyingine.

Hapo kabla Express zilikuwa zikiishia barabara kuu ya Makongoro - Airport kukwepa wananchi wenye hasira ambao walikuwa wakiziponda mawe Express zilizokuwa zikithubutu kupita barabara hiyo inayoishia darajani hapo (yaani nusu ya safari) na kuwapa usumbufu abiria wanao elekea maeneo ya mbali.



Ujenzi wa daraja hilo unaofanywa na mkandarasi Nyanza Roads ukiendelea usijulikane utaisha lini. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.