Tamasha la tano la Kilimanjaro Mtikisiko 2012 linalodhaminiwa na TBL kupitia bia yake murua ya
kilimanjaro Premium Lager na Vodacom tanzania na kuratibiwa na kituo cha redio Nyanda za juu kusini mwa Tanzania Ebony Fm limefana.
Tamasha hilo la kila
mwaka linalopita mikoa yote ya NYANDA ZA JUU KUSINI...weekend iliyopita (21st
Oct)..limeanzia katika mji mdogo wa MAKAMBAKO ambapo show mbili kali zilifanyika.
Show ya kwanza ikiwa
katika uwanja wa AMANI kuanzia saa nane mchana na ya pili kwenye ukumbi wa
GREEN CITY kuanzia saa mbili usiku ambapo wasanii AMINI, LINAH na ROMA waliweza
kukonga nyoyo za wapenda burudani wa MAKAMBAKO na vitongoji vyake.
Msanii na mkali wa vichekesho
kutoka ORIGINAL KOMEDI MPOKI alitegemewa pia kuonekana kwenye stage ya tamasha
hilo lakini hakutokea kwa sababu ya kuahirishwa kwa ndege asubuhi ya jumapili
alipokuwa Zanzibar kwenye show nyingine aliyokuwa amealikwa jumamosi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.