Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akizindua mradi wa maji. |
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akikinga maji mara baada ya ufunguzi wa mradi huo. |
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana amempa saa 24 Mkuu wa
Idara ya Maji wa wilaya hiyo kuwasilisha ripoti ya mradi wa maji uliojengwa
katika Kijiji cha Bugabu uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya Mwanza.
Amri hiyo ya Liana inatokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji
cha Bugabu wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi
ya shilingi million 5.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo wa maji
utakaosaidia wananchi wa vijiji vitatu, Jaqueline Liana amesema kumekuwa na
tabia kwa wakuu wa idara na viongozi wa vijiji kutosoma mapato na matumizi ya
miradi.
Amesema kuwepo kwa usiri katika miradi mbalimbali kunawafanya
wananchi kuichukia serikali yao, kitu ambacho kinaweza kuepukwa iwapo suala la
kusomwa mapato na matumizi litazingatiwa.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Bugabu Rebecca Jonas na baadhi ya
wananchi wa kijiji hicho wamezungumzia changamoto mbalimbali kuhusiana na mradi
huo wa maji.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Alpha Choice inayomiliki viwanda vya
kusindika minofu ya samaki katika nchi za Afrika Mashariki Bruno Mhoja amesema
mradi huo wa maji ni makakati wa kampuni kushirikiana na jamii katika miradi ya
maendeleo.
Mradi huo wa maji ni wa kwanza katika kijiji cha Bugabu kutolewa
na wawekezaji ambao utawanufaisha wananchi zaidi ya laki moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.