AFISA wa Uhamiaji ofisi ya Mkoa wa Mwanza Albert Buchafwe amenusurika
kuuawa kwa risasi baada ya kushambuliwa na Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Nyakato,
Abubakar Zebo kwa madai kuwa walikuwa wakishambulia jambazi.
Kamanda Liberatus Barlow. |
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza,
Liberatus Barlow linadaiwa kutokea majira ya saa 4: 13 usiku wakati afisa huyo
wa uhamiaji akiwa njiani kuelekea
nyumbani kwake ambapo alikutana na gari dogo aina ya Suzuki lililomuashia taa
likimuashiria kusimama.
Akielezea mkasa kamili Buchafwe alisema kwamba baada ya kuwashiwa alipochunguza
kwa makini gari hilo aliweza kulibaini kuwa ni lile linalotumika na afisa huyo
wa Polisi, hivyo alisimama na kujitambulisha kwake akiwa ndani ya gari lakini
aliamuriwa kuzima taa za gari lake na kutoka ndani yake.
“Nilitii nikazima taa, lakini nilisita kutoka katika gari langu,
nilijitambulisha kwamba mimi ni afisa Uhamiaji na kumtaja jina afisa huyo,
ambaye aliendelea kunilazimisha kushuka ndani ya gari huku nikiona akijiweka
sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa Bastora yake tayari kwa kushambulia,” alieleza.
Alisema wakati bado akijitambulisha alishuka askari aliyekuwa na sale
katika gari hilo la afisa huyo wa polisi akiwa na silaha ya SGM hali ambayo
ilimlazimu kugeuza gari haraka na kukimbia huku gari lake likishambuliwa nyuma kwa
risasi.
“Gari langu limeshambuliwa kwa risasi zaidi ya tano, moja imetoboa
upande wa mbele karibu na Taili ya kulia, risasi tatu zimetoboa nyuma ya gari
na moja ubavuni mwa gari upande wa nyuma, lakini sikuweza kupata madhara hali
ambayo ilinilazimu kukimbia hadi ofisini kwangu na kutoa taarifa kwa bosi wangu
wa mkoa usiku huo,” alizidi kufafanua.
Buchafwe alisema amepatwa na mashaka na tukio hilo kutokana na asakri
huyo aliyehusika kuwa na mahusiano ya karibu na mkewe ambaye wamekuwa na ugomvi
naye pamoja na kesi ya kutalikiana mahakamani na kusema kwamba huenda ahalikuwa
la bahati mbaya.
“Nina kesi na mke wangu mahakamani, na afisia huyu wa polisi amekuwa na
mahusiano ya karibu na mke wangu huyu ambaye tunashitakiana mahakamani,
inanishangaza kwamba mtu ambaye ananifahamu licha ya kujitambulisha bado
alikuwa akishilikilia msimamo wa kunitaka kushuka, nadhani hapa kuna jambo
zaidi ya hali ilivyo,” alieleza.
Aidha akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alikiri
kuwapo kwake na kudai kwamba anayo hakika kwamba tukio hilo limetokea kwa
bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiinterejensia za kuwapo kwa
majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na ambalo afisa huyo wa uhamiaji alikuwa
nalo.
“Hili ni tukio la bahati mbaya, jeshi laetu lilipata taarifa za
Kiinterejensia juu ya kuwapo kwa majambazi na kuamua kuweka mtego, sasa afisa
huyu alifika muda na wakati ambao askari wetu walikuwa eneo hilo na kuingia
katika mtego wetu, alikuja na gari ambalo ni sawa na lile ambalo tulielezwa
kuwa lingetumika, lakini bahati nzuri mauaji hayakutokea,” alifafanua kamanda
huyo.
Kamanda Barlow amedai kwamba kutokana na tukio hilo amepanga kukutana na
afisa huyo wa uhamiaji na kuzungumza naye akiwa na askari wake kutafuta suluhu
ya jambo hilo ambalo aliekeza kwamba yeye anaamini limetokana na bahati mbaya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.