ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 16, 2012

MAMA YETU MPENDWA MAREHEMU MARIAM SUNGURA ALIVYOZIKWA LEO HUKO MALYA WILAYANI KWIMBA MWANZA

Watoto wa marehemu wakiweka mchanga kwenye kaburi la mama yao mzazi marehemu Mariamu Sungura, kutoka kushoto ni Anton Dialo, Samwel Nyalla na David Nyalla.


Mwili wa marehemu Mariamu Sungura ukiwa ndani ya jeneza muda mfupi baada ya kushushwa kaburini.


Askofu wa kanisa la AICT wilayani Kwimba akisoma sala ya mazishi kwenye makaburi ya huko Malya wilayani Kwimba mkoani Mwanza.


Kutoka kushoto ni Seleman Fish, David Nyalla (mtoto wa marehemu) na Dj Maliz


Watoto wa marehemu Maria Sungura kutoka kushoto ni Samwel Nyalla, Anthon Dialo na baadhi ya wajukuu na waombolezaji wakifuatilia mazishi.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Clement Mabina akiweka shada la maua juu ya kaburi.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kwimba Peter Ng'hingi akiweka shada la mauwa kuwakilisha wanachama na viongozi wa CCM wilaya ya Kwimba.


Mkuu wa wilaya ya Kwimba Seleman Mzee akiweka shada kuwakilisha viongozi wa serikali wilaya ya Kwimba.


Kutoka kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Daniel Ole Porokwa akiweka shada la maua na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Seleman Khamese


Mkurugenzi wa mgahawa wa Pizeria na wadau kutoka Magu, Misungwi na Mwanza wakimfariji Mkurugenzi wa Sahara media Group Anthon Dialo mara baada ya maziko ya mama yake mzazi.


Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM mkoa wa Mwanza (UVCCM) Boniface Magembe, katibu wa UVCCM mkoa wa Mwanza Elias Mpanda na katibu wa UVCCM wilaya ya Ilemela Mabiha.


Mwakilishi wa serikali mkoa wa Mwanza Doroth Mwanyika ambaye ni katibu tawala wa mkoa (RAS) akiteta jambo na katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga na kushoto kabisa ni katibu wa Madiwani wa CCM Halmashauri ya jiji la Mwanza Sarah Ng'wani.




Wadada na wafanyabiashara maarufu wa maduka ya Nguo na urembo jijini Mwanza nao walikuwepo kama kamera ya blogu hii ilivyowanyaka.


Meneja wa kampuni ya Simu za Mkononi Airtel Kanda ya Ziwa Ally Maswanya (Kushoto)  na kulia kabisa ni Six Kisuruli mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza.


Huyu ni Mtoto wa Kwanza wa marehemu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki Star Tv, Kiss Fm, Radio Free Afrika, Gazeti la Msanii Afrika na Uchapishaji majarida mbalimbali hapa jijini Mwanza akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu mama yake
PICHA ZOTE NA PETER FABIAN WA g sengo blog.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.