ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 15, 2012

AIRTEL YATANGAZA SHULE 93 ZA SEKONDARI ZITAKAZONUFAIKA NA MRADI VITABU AIRTEL SHULE YETU TANZANIA NZIMA

Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama ' AIRTEL SHULE YETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo. Kulia  anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi na Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda (shoto). Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110

Shule 3 kutoka katika kila mkoa kupata msaada wa Vitabu toka Airtel Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanoyo kama ' AIRTEL SHULE YETU' iliyofanyika katika ofisi za Airtel na kupata shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huo.

Kulia  anaefuatilia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi
Airtel yatangaza shule  93 za Sekondari Kufaidika na mradi wa Vitabu
.       Shule 3 kutoka katika kila mkoa kupata msaada wa Vitabu toka Airtel
.       Airtel kutumia zaidi ya milioni 110 kwa ajili ya Vitabu mwaka 2012 -2013



Dar as Salaam, Airtel Tanzania, leo imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari  93 zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama  Airte shule yetu kwa  mwaka 2012 -2013 Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Mwaka huu
, Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule  za sekondari 93, Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.

Shule 93 zilizo chaguliwa leo ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu.

"Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani  kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.

Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule  iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya Bi Mallya aliongeza kwa kusema "tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa  kuwapatia vitabu vya mitaala ya  masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara"

"Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania  hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu  kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh  kwa  shule za sekondari kwa kupitia  droo iliyohusisha jumla ya shule 502" alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema "Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini " Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu  na maisha ya watanzania"

Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini" aliongeza kwa kusema Bw, Nyirenda Mbali na  shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu.

Pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.
Mwisho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.