Waziri wa Mali asili mh Balozi Khamisi Kagasheki akitoa ufafanuzi kwa wananchi katika mkutano huo. |
Waziri wa Mali asili mh Balozi Khamisi Kagasheki akitoa ufafanuzi kwa wananchi katika mkutano huo. |
Maafisa wa Jeshi la Polisi Wilayani Serengeti wakiwa katika mkutano huo. |
SERENGETI
SERIKALI imesema
haitasita kuchukua hatua za kuzifunga kambi zote za kitalii ambazo zimo katika
maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama pori WMA,ambazo zitaendelea kukiuka
sheria na Kanuni kwa kulipa mapato yatokanayo na shughuli ya utalii kwa uongozi
wa vijiji badala ya malipo hayo kufanyika kupitia WMA.
Agizo hilo limetolewa
na waziri wa Maliasili na Utalii Mh Balozi Khamis Kagasheki,wakati akizungumza
na viongozi wa WMA ya Ikona wadau wa sekta ya utalii katika wilaya ya Serengeti
mkoani Mara.
Amesema hivi sasa
kumeibuka migogoro kwa baadhi ya WMA kwa kuhusisha viongozi na wananchi wa
vijiji husika ambayo imekuwa ikihatarisha amani na mahusiano kati ya kijiji na
kijiji kwa kugombea mapato baada ya baadhi ya kambi za utalii kukiuka kanuni na
kwa kulipa tozo hizo moja kwa moja kwa baadhi ya serikali za vijiji kinyume cha
sheria.
Waziri
Kagasheki,alifikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa mgogoro ambao umekuwa
ukiendelea katika WMA ya Ikona wilayani Serengeti umechangiwa na baadhi ya kambi
za kitalii kulipa mapato yake kwa baadhi ya vijiji wakati wakitambua wazi kuwa
kambi hizo ziko ndani ya eneo la WMA.
Kwa upande wao baadhi ya
wananchi na viongozi wa vijiji vitano vinavyounda WMA ya Ikona,walimesema
mgogoro huo pia umechangiwa na uongozi wa WMA kushindwa kusoma taarifa za mapato
na matumizi kwa wananchi,madiwani kujineemesha huku wananchi wakishindwa kuvuna
mazao mashambani baada ya kushambuliwa na wanyamapori kutokana tu na kuthamini
shughuli za uhifadhi.
WMA ya Ikona inaundwa na vijiji vya Nyatambiso,Park Nyigoti,Nyichoka,Makunduzi na Rubanda ambapo tayari WMA 38 zimeanzishwa nchini 17 zikiwa zimetangazwa rasmi katika gazeti la serikali lengo likiwa kuhakikisha wananchi wanahifadhi na kunufaika na raslimali hiyo kwaajili ya kupunguza umasikini miongoni mwao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.