Mmarekani Chris wilde aahidi kurudi
mwakani
Chris Wilde raia wa Marekani aliyekimbia kilometa 50 kuipa Tanzania zawadi ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ameahidi kurejea tena mwakani kukimbia kilometa 51 katika mbio za kutimiaza miaka 23 tangu kuanzishwa kwa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
Simama mahala alipomalizia mbio za kilometa 50 kama zawadi kwa uhuru wa Tanganyika. Kulia kwake ni mkimbiaji wa kimataifa wa Tanzania Nelson Brighton |
Wilde
ambaye ni mganga msaidizi kutoka jimbo la Minnesota amekuwa mtu wa kwanza
kukimbia kilometa 50 kusheherekea uhuru wa Tanganyika alipokimbia katika mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathon jumapili tarehe 24 mjini Moshi.
Mbio
hizo zilifanyika kuanzia Moshi Club hadi Rau madukani na kurudi. Chris Wilde
alirudi mara 9 na nusu ili kutimiza kilometa 50 kama zawadi kwa nchi ya
Tanzania.
“Naipenda
sana Tanzania na ili kuidhihirishia dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko Tanzania,
nakimbia mbio hizi kama zawadi kwa Tanzania” alisema mzungu huyo mwenye umbo la
mwariadha wakati anajiandaa kukimbia mbio hizo jumapili tarehe juni
24.
Wilde
aliongozana na mwanariadha wa kimataifa mtanzania Nelson Brighton na ambaye
anakwenda nchini Marekani mwezi ujao kushiriki katika mbio mbalimbali
zilizoandaliwa kwa ufadhili wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991.
Kumiminika
kwa wakimbiaji wa Kimarekani, Ulaya, Australia, Canada na Scandinavia katika
mbio za Mt. Kilimanjaro marathon ni neema kubwa kwa taifa hili ambalo lina
hazina kubwa sana ya wanamichezo wanaotakiwa kuendelezwa.
Chris
Wilde aliungana na mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki
katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kuzifanya kuwa mbio zinazovutia
washiriki wa Kimataifa. Mt. Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na
Marie Frances kutoka Bethesda nchini Marekani.
Ni
mbio zilizokwisha kupewa tuzo na majarida mbalimbali yanayoheshimika duniani
kama vile Wonders of World ambalo lina wasomaji zaidi ya milioni 5 ambalo
lilizipa nafasi ya pili wakati ambapo jarida linaloheshimika la Forbes lilizipa
nafasi ya kwanza kama mbio zinazovutia.
Imetumwa
na;
Grace
Soka
Afisa
UhusianoMt. Kilimanjaro Marathon 1991
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.