ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 2, 2012

MASANJA MKANDAMIZAJI, KHADIJA KOPA, CHEGE NA TEMBA KUPAMBA REDDS MISS SHINYANGA 2012 ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI 7/07/2012 MJINI KAHAMA

Kwa mara nyingine tena Asela promotion inakuletea Reds Miss Shinyanga 2013 itafanyika katika uwanja wa Taifa Kahama mjini sikuu ya saba saba tarehe 7/07/2012 kuanzia saa mbili usiku. Mc atakuwa Masanja mkandamizaji toka Orijino Komedi, burudani kushushwa na wakali kama Khadija Omar Kopa, Chege na Temba pamoja na wakali kibao kutoka Mwanza.

Kiingilio VIP first class -Tsh 30,000/=
VIP two - Tsh 15,00/=
Kawaida - Tsh 5,000/=
 
Warembo wa Miss Shinyanga 2012 itakayorindima wilayani Kahama jumamosi hii ya tarehe 7/07/2013 uwanja wa Taifa Kahama.
Warembo hawa watahusika vilivyo kwa skilz zao, maandari ya eneo husika kupambwa na taa maalum, stage la uhakika na sound ya mtikisiko kurindima katika kusapoti burudani na yatakayojiri siku hiyo.

Warembo wameahidi kuonyesha ujuzi zaidi kwaajili ya kuuthibitishia umma wa Watanzania kwamba si sura pekee, haiba na mvuto tu walivyo navyo ni silaha kwenye harakati za maendeleo ya jamii yetu bali pia weredi unachangia na hakika wanajivunia kuwa nao wakutosha nao wanaahidi kuudhihirisha siku ya kinyang'anyiro cha Miss Shinyanga 2013 kitakachofanyika mji wa dhahabu Kahama.

Warembo katika pozi style.com

Coca cola ni moja kati ya wadhamini wakuu wa shughuli nzima.

Waremmbo na kinywaji chao katika pozi

Kutokana na maandalizi yaliyofanywa mpaka sasa na msisimko unaotajwa kinyang'anyiro hiki kinatajwa kuwavuta mashabiki toka sehemu mbalimbali nchini wengi wakitaka kushuhudia live bila chenga mpango mzima utakavyokuwa.

Baadhi ya warembo wa kinyang'anyiro cha miss Shinyanga 2012 wakikulingishia tabasamu zao.
Miss Shinyanga 2012 ni chini ya Udhamini wa Reds Premmium Cold, Nyamizi Secretarial, Club Dimpoz, Mongo Hotel, Beta Bidding Ltd, Zasco East Africa Ltd, CRDB Bank, Gazeti la Jambo Leo, Star Tv, Clouds Fm na G.Sengo Blog. 

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.