ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 1, 2012

DRT HARISSON MWAKYEMBE SERIKALI KUBORESHA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI TZ

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

SERIKALI imesema kuwa ipo kwenye mchakato wa kuviboresha viwanja mbalimbali vya ndege hapa nchini ukiwemo uwanja wa ndege wa Arusha kwa kuufanyia matengenezo makubwa uweze kuruhusu kutua kwa ndege kubwa za kimataifa.

Waziri wa uchukuzi ,Dkt Harisson Mwakyembe aliyesema hayo jana baada ya kupokea taarifa fupi wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya kufanya ziara fupi mkoani hapa.

Dkt Mwakyembe alisema kuwa uwanja wa ndege wa Arusha unaumuhimu wa kipekee katika kuendeleza utalii wa ndani na kueleza kuwa serikali itafanya kila njia kuhakikisha kuwa uwanja huo unapanuliwa na kuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa.

Alisema amekuwa akipata malalamiko mengi kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kunyangánya wateja wa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) huku maombi hayo yakitaka uwanja huo ufungwe.

‘’nimepata taarifa za kutaka kufungwa kwa uwanja huu wa ndege wa Arusha kwa kuwa unatumika kunyangánya abilia wa uwanja wa KIA, nimejiridhisha kuwa kiwanja hiki kina umuhumu wa kipekee na serikali itaangalia uwezekano wa kukiboresha’’alisema Mwakyembe.

Alisema serikali itatenga fedha zaidi kwa ajili ya kukiboresha kiwanja hicho ili kiwe cha kisasa zaidi ,ikiwa ni pamoja na kuviboresha viwanja vingine vya Songwe,Kigoma na Mwanza.

Awali Kaimu mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha Arusha,Mhandisi Suleiman Suleiman alisema kuwa kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa eneo la maegesho ya ndege, jengo la abilia na jengo la zima moto.

Alisema changamoto zingine ni pamoja na kutokuwa na taa zinazowaka majira ya usiku hivyo kutoruhusu ndege kutua ama kuruka nyakati za usiku,kituo cha umeme ,Mnara wa kuongozea ndege ,Jengo la hali ya hewa, jengo la Mizigo pamoja na miundombinu yake.

Aidha alisema kuwa ukarabati wa kiwango cha lami wa barabara ya kuruka na kutua yenye urefu wa mita 420 uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7umefanya urefu wa barabara hiyo kufikia mita 1620 hivyo kuwezesha ndege zenye ukubwa wa kubeba abilia 70 kuweza kutua katika kiwanja hicho.

Mhandisi Sulemeni aliongeza kuwa kwa sasa kiwanja hicho kinahudumia wastani ndege 1700 kwa mwaka na abilia wanaohudumia kwa mwezi ni 12,000.

Alisema kuwa mpango wa sasa ni kuhamisha barabara ya Arusha Babati na tayari wamemweleza wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads).

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano uliopo sasa, pamoja na kuhamisha barabara ya sasa ya kuingia kiwanjani hapo kwaniinaingiliana na maegesho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment