Na Shomari Binda
Musoma,
Watu wa Wanne wanasadikiwa kuwa ni majambazi walioshiriki katika tukio la kuwavamia wachimbaji na wanunuzi wa Dhahabu katika Kijiji cha Magunga kata ya Buhemba Wilaya ya Butiama na kuwaua watu watano wamefikishwa mahakamani hii leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara nakusomewa mashitaka ya mauaji katika kesi Na 13 ya mwaka 2012.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Janeth Musaloche imedaiwa kuwa mnamo June 2 Mwaka huu katika Kijiji Cha Magunga washitakiwa hao wanne kwa pamoja waliwavamia Wananchi wakiwa katika shughuli zao za Biashara wakiwa na risasi za moto pamoja na mapanga na kuanza kuwadhuru Wananchi hao na kupelekea Mauaji ya watu watano.
Watu hao wanne waliopandishwa kizimbani kwa makosa hayo ni Alex Jerry (45)mkazi wa mtaa wa Majita katika Manispaa ya Musoma,Chacha Mtatiro (37 mkazzi wa Msati Mugumu,Amiri Musa Sibitali (38) mkazi wa Mwisenge darajani Manispaa ya Musoma na God Jackson (26) mkazi wa Sirari katika Wilaya ya Tarime.
Waliofariki katika tukio hilo ni Charles Jaoko Orengo wa Buhemba,Nyamhanga China Magige wa Tarime,Joseph Chacha Nchago wa Tarime,Juma Marwa Chacha wa na Kiraryo Gungwa wa wakazi wa Mirwa Wilaya ya Musoma Vijijini.
Watuhumiwa wote wanne katika kesi hiyo hawakutakiwa kujibu chochote wakisubili Mahakama kuu kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na imehairishwa hadi Julai 4 huku watuhumiwa hao wakirudishwa Rumande.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.