ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 14, 2012

WAIGIZAJI WA FILAMU WAFARIJIKA KUFANYIKA KWA TUZO ZA FILAMU MWAKA HUU


Mwigizaji wa filamu Irene Uwoya akiongea mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutangaza tuzo za filamu zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini TUZO hizo za kwanza kabisa za waigizaji wa filamu zimepangwa kufanyika mwezi ujao, Mratibu wa kampuni ya Bantu Film Award, Stuart Kambona amesema, Mkutano huo umefanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.  Mwigizaji Irene Uwoya amewapongeza waandaaji hao kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo alisema zitawapa changamoto kwao kuandaa filamu za ushindani. Pia alishukuru kampuni ya Bantu kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo anaamini zitawafanya kuandaa filamu zenye ubora wa hali ya juu.

Waandishi wa habari wakiadika mambo muhimu yalioongelewa katika mkutano huo

Mwigizaji Rich Mtambalike naye alipata nafasi ya kuzungumza machache katika mkutano huo na kushukuru waandaji kwa kuanzisha tuzo hizo ambazo zitatoa nafasi kubwa kwa waigizaji wa filamu, waandishi wa filamu na waongozaji wa filamu kujitangaza kitaifa na kimataifa

Mwigizaji Jacob Steven akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.