Kaike Promotion
imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati BAINA MAZOLA na JUMA
FUNDI (ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini Philipines)
litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa saba,pambano hili ni mtiririko
wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi
na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya
dunia.
Inafahamika wazi kwa taifa letu, mchezo wa ngumi ni miongoni mwa
mchezo unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio
na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila
ya utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na
mchezo unaohitaji msaada wa hali ya juu sana
kuinuliwa.
Wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa
letu. Mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na TPBO na mapambano yamepangwa
na Ibrahim Kamwe chini ya uratibu wa Kaike Siraju yataongozwa na mapambano
ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi Issa Omar (toka bigright
boxing Mwananyamala) na Ramadhan Kumbele bingwa wa taifa toka kambi ya
Matumla -Keko.
Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi Mwaite Juma (toka bigright boxing)
Mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini na katika picha ni Issa Omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright
Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title
Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round
Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round
Super feather weight - Doi Miyeyusho v/s Shaban Mtengela 6 round
light weight - Bakari Mohamed v/s Sadiki Momba - 6 round
DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.