ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 11, 2012

MISS UTALII TANZANIA 2012 - KANDA YA ZIWA KUFANYIKA TAREHE 30 JUNI

Shindano la kumsaka Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, litafanyika tarehe 30 Juni 2012 , katika ukumbi wa Monarch Hotel Mwanza. Shindano hilo linaloandaliwa na Fania Hassani ambaye ni mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation - Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Fania Beauty Entertainment litashirikisha Jumla ya warembo 15 kutoka mikoa ya Mwanza,Kagera na Geita na Kigoma, ambayo kwa mujibu wa mgawanyo wa kanda a mashindano ya Miss /binti Utalii Tanzania ndiyo mikoa ya kanda ya ziwa ya mashindano hayo. Huku mikoa ya Simiyu,Mara na Shinyanga ikiwa ni Kanda ya Magharibi ya mashindano hayo.

 
Warembo wote wameanza kambi ya mazoezi katika hoteli hiyo ya Monarch Hotel Mwanza, wakiwa chini ya ukufunzi wa Rose Mary Kasiga Miss Utalii Mwanza 2011 na Fania Hassani Miss Utalii Dodoma 2007.

Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii kanda ya Ziwa 2012 wakiwa kambini Monarch Hotel

Wadhamini wakuu wa shindano hilo la Miss Utalii Kanda ya ziwa 2012 ni kampuni ya Gold Master, huku wadhamini wengine wakiwa ni hoteli ya kitalii ya Monarch Hotel ya mjini Mwanza, magazeti ya Jamboleo, Kiu na misstourism.blogspot.com.

Aidha waandaaji wameomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ,ambalo ni la pekee na lenye manufaa makubwa kiuchumi na kitamaduni kwa kanda ya ziwa na taifa kwa ujumla, kwani tofauti na mashindano mengine Miss Utalii tanzania linalenga kutangaza na kuhamasisha utalii, utamduni, mianya ya uwekezaji, elimu, afya ya jamii, maliasili za taifa, mazingira, bidhaa za Tanzania na vita dhidi ya uwindaji haramu, uvuvi haramu, mila kongwe na potofu.

Washindi wa shindano hilo watawakilisha mikoa ya kanda ya Ziwa katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012, ZITAKAZO FANYIKA NOVEMBA 2012

Asante,
Fania Hassani - Mkurugenzi Miss Utalii Kanda ya Ziwa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.