ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 30, 2012

TUNAITAJI UKUMBI BORA WA MASUMBWI


Mchezo wa ngumi katika nchi yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi kutokana na kuchipuka kwa mabondia wengina mapromota ambao wanapigana katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na kuandaa mapambano . wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .

Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje ya Tanzania kama Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa Ally Kimweri na Emanuel Mrundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo. jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini nimeona jumatatu ya leo nijaribu kulitilia mkazo .

Natoa mfano kama tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil basi hata mchezo wa ngumi linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.

Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO,KBF bila kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa mchezo huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa mpira wa miguu ambao hata Suleiman Nyambui anafaidika nao halikadharika wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama ilivyo Las Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri inawezakana kwa Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama vya mchezo wa ngumi vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana na serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha tunapata kumbi bora ya kisasa ya kupigania ili kuongezea ujuzi na viwango vya mchezo wa ngumi kwa Tanzania.

Kama Ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata Tanzania inaweza pia kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo pekee ambao unakuja kwa kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye mwaka jana alitunikiwa tuzo ya heshima ya mwanamichezo na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA kuwa kiongozi bora kwa kujari michezo si vibaya Mh Jakaya Kikwete akatuachia wapenzi wa masumbwi kumbi bora w hata mabondia wanje wajekupambana Tanzania kama zinavyokuja timu kubwa za mpira dunia kucheza uwanja wa taifa .

Nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini na kuupanua mchezo huo na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania katika Nyanja za utalii ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wa wakubwa wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa Tanzania .

Na: Super D Boxing Coach
www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.