Monday, April 09, 2012
AJALI
Taarifa tulizopata muda mchache uliopita kutoka mkoani Kigoma zinasema kuwa ndege ya Shirika la ATC imepata ajali muda mchache uliopita huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mvua zilizonyesha na hata kusababisha run way kutengeneza tope hata ndege kushindwa kuruka wakati ikitengeneza mwendo kasi wa kuruka.
Inatajwa kuwa hadi ilipofika ukingoni yaani mwisho mwa run way, ikakatika bawa lake la kulia.
Pia imethibitika kuwa ndege hiyo imeanguka wakati ilipokuwa inataka kupaa kwenye uwanja wa ndege Kigoma ikiwa na Abiria wote 35 ambao wote wamenusurika na wako salama.
ENDELEA KUFUATILIA KWA TAARIFA ZAIDI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.