Ajali hiyo imetokea katika mtaa wa Kitangiri Jijini Mwanza wakati akiwa safarini kwenda kituo cha kazi huku akiwa amepanda kwenye Pikipiki na kufika eneo hilo ambapo Nondo hizo zilikuwa zikipakiwa kwenye gari (Pick up) moja eneo la Kitangiri Mwanza ambayo baada ya kurushwa nao wakiwa wamefika eneo hilo iliruka hadi upande wa barabafra na hivyo kuingia ndani ya jicho lake la kushoto na kumjeruhi vibaya.
Kwa Mujibu wa Henry Kavilondo tukio limetokea majira ya saa 10: 45 Jioni Machi 26 Mwaka huu, ambapo wakati akiwa amepanda pikipiki ambayo ilipita jirani na gari hiyo ambayo ilikuwa imepaki kwenye eneo la barabara ikipakiwa nondo, na ghafla mpakiaji alirusha nondo moja ambayo iliteleza na kuangukia upande wa pili na alikumbana nayo uso kwa uso wakati pikipiki iliyokuwa imembeba ilipokuwa ikipita.
Kutokana na ajali hiyo kwa sasa yupo katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu lakini Madaktari wanaeleza kwamba jicho lake limeshaharibika hivyo walilazimika kuliondoa na kumfanya kuwa mlemavu wa jicho moja kutokana na jicho hilo kuondolewa leo jana kwa kufanyiwa upasuaji ili kunusuru jicho lake la upande wa kulia nalo lisiharibike.
Mpiga picha huyu kwa bado amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza wodi Namba J4-Chumba 404 kwa matibabu, blogu hii kesho inaahidi kufanya mahojiano maalum na Mwandishi huyo.
Habari na F.Katulanda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.